Zaidi ya Dola milioni 1.8 za kimarekani sawa na wastani wa Shilingi Bilioni 4.3 za Kitanzaia hutolewa kila mwaka Kwa wanavijiji 11 vinavyouzunguka Mgodi wa Barrick North Mara tangu mgodi huo uanze kuendeshwa na kampuni hiyo kubwa ya uzalishaji wa Madini Duniani
Kiasi hicho cha fedha kinatumika pia kufanikisha miradi ya kimkakati kama vile barabara, maji, ukarabati na ujenzi wa shule, uikarishaji huduma za Afya nakadharika
Aidha mgodi huo umesababisha uwepo wa ongezeko kubwa la ajira kwa wananchi, utoaji wa zabuni kwa kampuni za wazawa wilayani Tarime ambapo zaidi ya kampuni za wazawa 55 hutoa huduma mgodini hapo na kulipwa Mabilioni ya Shilingi kila mwezi.
Aidha Kwa kipindi Cha miaka hii mitatu umeajiri zaidi ya watu 2,923 katika nyanja tofauti huku asilimia 96 ya watu hao wakiwa ni watanzania huku zaidi ya asilimia 98 ya watumishi wa Makampuni yanayotoa huduma mgodini hapo wakiwa ni wazawa
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Barrick North Mara, Francis Uhadi alisema mafanikio ya mgodi ni kuajili wananchi wengi ambapo kwa asilimia 46 ya watu walioajiriwa mgodini ni wale wanaozunguka mgodi huo.