Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwenye Jukwaa wakati Wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Mama Maria Nyerere wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakipiga ngoma kabla ya kuingia Rasmi katika Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Rasmi la Ukaguzi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson pamoja na Spika wa Baraza la Waakilishi Mhe. Zubeir Ally Maulid mara baada ya kufungua Jengo la Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Viongozi wa Serikali, Viongozi wastaafu, watu mashuhuri pamoja na wananchi wengine wakiwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu Chamwino tarehe 20 Mei, 2023.
….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani amefanya ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Ikulu Chwamwino, Dodoma
Katika ufunguzi huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameshiriki katika Ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Ikulu Chwamwino, Dodoma
Ufunguzi huo uliongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao Tanzania na Wananchi wa Mikoa yote ya Tanzania.