Na MWANDISHI WETU
MENEJA wa Kanda ya Ziwa wa Bohari ya Dawa (MSD) Egidius Rwezaura, ameswma hivi karibuni wanatarajia kupokea vifaa vya afya zikiwemo dawa na vifaa tiba aina 100 ikiwemo vitanda na mshine za maabara ambavyo vitamaliza changamoto ya mahitaji yaliyopo.
Rwezaura, ameswma hayo jana akizungumza katika kikao kazi na watendaji wa sekta ya afya wakiwemo waganga wakuu na Wafamasia wa mikoa na wilaya, wataalamu wa maabara na waganga wa vituo vya afya na hospitali za serikali za kanda hiyo mkoani Mwanza.
Pia alisema mkakati ni kuwapo vifaa vingine vingi vya akiba katika bohari, kufikia lengo la Rais Dk. Samia katika maboresho ya huduma sekta ya afya nchini.
Naye Mfamasia Mratibu Kiongozi wa Huduma za Bidhaa za Afya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mathew Mganga, alisema watendaaji hao watambue kuwa Rais ametoa fedha nyingi za dawa na vifaa ni vyema zitumike katika ununuzi wa bidhaa hizo na sio matumizii mengine.
Alisema lengo la maboresho sekta hiyo, ni kufanikisha huduma bora kwa wananchi ambapo bado fedha zinazomiminika na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Rais Dk.Samia haiendani na huduma bora wanazopatiwa wananchi hivyo ni lazima kuchukua hatua.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk.Zabron Masatu, alisema wamepokea maelekezo hayo wataenda kubanana ndani katika utendaji kuweza kufikia lengo la Rais katika maboresho ya huduma bora za afya kwa wananchi.