Wakati serikali ikithibitisha kutoa Bil 15.4 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi waliyopisha migodi ya Liganga na Nchuchuma wilayani Ludewa hatua ambayo ni maandalizi ya kuanza machimbo hayo ,Wakazi wilayani humo wameitaka serikali kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya madini yatakayoanza kuchimbwa ikiwa ni pamoja na Chuma,Titaniam na Vanadiam yanayopatikana katika migodi hiyo ili kutengeneza ajira kwa vijana badala ya kusafirisha kwenda kuyaongezea thamani katika mikoa mingine ama nje ya nchi.
Mbali na kuomba kujengwa viwanda vya kuongeza thamani ya madini hayo,wananchi hawa pia wameitaka serikali kupitia shirika la maendeleo ya taifa NDC kutekeleza makubaliano waliyoweka miaka ya nyuma ya ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kisha kusambaza kwa wananchi.
Wakiweka bayana matamanio yao katika mkutano wa hadhara uliyoitishwa na mkuu wa mkoa wa Njombe katika kijiji cha Nkomang’ombe ukiwa na lengo la kueleza juu kuanza ulipaji wa fidia kwa waliyopisha migodi na kisha kutoa elimu juu ya matuzi bora ya fedha kiasi cha bil 15.4 wananchi hao akiwemo Simon Muhagama wamesema ni kiu yao ya muda mrefu kuona madini yaliyolindwa wazee wao yanaanza kuchimbwa hivyo kabla ya kuanza machimbo hayo ni vyema serikali ikajenge viwanda vya kuongeza thamani na mtambo wa kuzalisha umeme ili wakazi wa Ludewa wanufaike hazina hiyo pamoja na ajira.
Kuhusu fidia wamesema mchakato unakwenda vizuri kwasababu serikali imekubali kufidia hadi makaburi ya wapendwa wao na kisha kutoa ombi kwa serikali kuboresha huduma za kijamii katika Kijiji cha Idisi ambacho wanapaswa kuhamia kwa kuwa hakina shule Wala Zahanati.
“Kwa muda mrefu wakazi Ludewa wamekuwa wakitaka machimbo ya makaa wa mawe na chuma yaanze kufanyika lakini imekuwa ngumu Ila kipindi hiki rais Samia ameamua kulipa Fidia na kuanza kichimba,mwenyekitinwa CCM wilaya ya Njombe Stanley Kolimba.
Akitoa ufafanuzi kuhusu maswali ya wananchi ofisa mwandamizi wa shirika la maendeleo la Taifa NDC Frolian Mlamba amesema wakati wawekezaji watano wakitarajiwa kuanza machimbo katika migodi hiyo serikali pia inaendelea mazungumzo na muwekezaji wa china juu ya ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamani madini Ili kuzalisha bidhaa za chuma katika wilaya ya Ludewa Jambo ambalo litasaidia kutengeneza ajira kwa wananchi.
Kwa niaba ya taasisi za kifedha meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Nyanda za juu kusini Jenipher Tondi amesema benki yao imeona umuhimu wa kutoa elimu ya fedha kwa wanufaika wa Fidia kabla hawajalipwa ili waweze kutumia fedha hizo vizuri kwa kubuni miradi Kama ujenzi wa Hoteli za Kitalii na nyumba za kulala wageni maeneo yenye hazina ya Madini ili kutengeneza kipato zaidi.
Tondi amesema wamelazimkka kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa Mkomang’ombe na Mundindi Ludewa kwasababu Kama hawatapatiwa huduma hiyo fedha hizo zitatumika vibaya na kurejesha malalamiko kwa serikali.
“Niwaombe wekeni fedha kwenye mabenki Pindi mtakapolipwa kwasababu kukaa nazo nyumba Kuna hatarisha usalama hivyo rai ni kuweka fedha katika benki ya CRDB.
Punde baada ya kusikia mapendekezo ya wananchi punde baada yankuanza machimbo mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema njia pekee ya kunufaika na Fidia hiyo ni kuanzisha miradi mipya ya kouchumi Kama sheli, grocery,Hoteli na nyumba za kulala wageni .
Mtaka ametoa onyo pia kwa matapeli watakaoibuka katika vijiji vya mradi kuwaibia wananchi huku pia akisema fedha hiyo isiwe chanzo Cha kufarakanisha familia na Koo kwani ni ya kupita.