…………………
Na Victor Masangu,Kibaha
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Abdalah Shaib amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuweza kuchochea maendeleo ya wananchi katika nyanja mbali mbali ikiwemo elimu pamoja na afya.
Pongezi hizo amezitoa mara baada ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ikiwemo kuweka jiwe la msingi katika maktaba na jengo la utawala katika shule ya sekondari Mwambisi forest.
Kiongozi huyo alibainisha kwamba ameridhishwa na mradi huo na kudai kumetokana na juhudi mbali mbali zinazofanya na Baraza la madiwani,kwa kushirikiana na Mbunge wao kwa lengo la kuweza kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo
Aidha kiongozi huyo wa mbio za Mwenge alimpongeza mkuu wa Wilaya ya Kibaha pamoja na jopo lake lote kwa kuanzisha miradi ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia wananchi.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akitoa salamu zake kwa kiongozi wa mbio za Mwenge alisema kuwa katika shule hjyo ya Mwambisi alishachangia kufanikisha mradi wa ujenzi wa darasa moja ili Wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki.
Kadhalika Mbunge huyo aliongeza kwamba ataendelea kusaidia na kuchagiza kasi ya maendeleo kwa wananchi wa Jimbo lake katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu,afya,maji,miundombinu ya barabara na huduma nyingine za kimaendeleo.
Nao baadhi ya wananchi wamepongeza ujio wa Mwenge wa Uhuru ambapo wamesema unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuzindua miradi na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbali mbali ya maendeleo na mingine imepata fursa ya kuetembelewa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya Kibaha mji zimeweza kukagua na kupitia miradi 12 ya maendeleo katika nyanja tofauti zikiwemo,afya,elimu,maendeleo ya jamii,barabara sambamba na mapambank dhidi ya madawa ya kulevya,ukimwi,rushwa,na malaria.