Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la kumi la Kisayansi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Self Shekalaghe lililofanyika leo tarehe 17/5/2023 katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala, Fedha na Mipango, Prof. Erasto Mbugi akizungumza jambo katika Kongamano la kumi la Kisayansi lililofanyika leo tarehe 17/5/2023 katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wakiwa katika Kongamano la kumi la Kisayansi lililofanyika leo tarehe 17/5/2023 katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es Salaam.
…..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania imeendelea kutekeleza mpango kazi wa Taifa wa kupambana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa (National Action plan on antimicrobial resistance (NAP -AMR) 2023-2028) katika mfumo shirikishi wa Afya Moja ‘One- Health approach’.
Mpango kazi huo umeainisha afua mbalimbali na malengo ya kimkakati katika kupunguza kasi ya usugu ambayo ni kuelimisha na kujenga uelewa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa, utafiti na ufuatiliaji, uzuiaji wa maambuki ya vimelea vya magonjwa, matumizi sahihi ya dawa.
Akisoma totuba ya ufunguzi katika Kongamano la 10 la Kisayansi leo tarehe 17/5/2023 kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Self Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, amesema kuwa usugu wa vimelea dhidi ya dawa husababishwa na matumizi mabaya au holela ya dawa dhidi ya vimelea kwa binadamu na kwa wanyama.
“Kama vile utumiaji ya dawa dhidi ya vimelea bila ushauri wa wataalamu wa afya, kutumia dawa bila kufanya uchunguzi wa vipimo vya maabara ili kujua dawa sahihi, kutokumaliza dozi kutokana na maelekezo ya wataalamu wa afya, kwa ujumla ni matumizi mabaya ya dawa kwa binadamu na wanyama” amesema
Amebainisha kuwa twakwimu zinaonyesha kuwa, matumizi ya dawa dhidi ya vimelea nchini yanakadiriwa kufikia 62.3% wakati makadirio ya usugu ni asilimia 59.8% katika sekta ya afya ya binadamu.
*Makadirio haya yanadhaniwa kuwa makubwa zaidi katika sekta ya mifugo na uvuvi ambapo tafiti zinaonyesha asilimia 90% ya wafugaji wanatumia dawa dhidi ya vimelea kutibu wanyama badala ya chanjo” amesema
Prof. Nagu amesisitiza kuwa katika vituo vya afya watumie maabara kujua maambukizi kwa wagonjwa kabla ya kutoa dawa dhidi ya vimelea.
“Hii itazuia matumizi holela na hivyo na kupunguza usugu dhidi ya dawa, vivyo hivyo, napenda kutoa ushauri na kuwaelekeza pia wenzetu wa sekta ya mifugo na uvuvi kusimamia maelekezo haya yaliyopo katika mpango kazi wa taifa”
Amesema kuwa mpango wa serikali ni pamoja na kuhakikisha kuwa wafugaji wanawatumia wataalamu wa mifugo na kuzingatia ushauri wanauotoa katika matumizi ya dawa.
Prof. Nagu amefafanua kuwa usugu wa vimelea dhidi ya dawa ni janga linaloikabili dunia kwa sasa, hivyo Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani, kwa kiasi kikubwa inakabiliwa na janga hilo usugu wa vimelea dhidi ya dawa.
Amesema kuwa changamoto iliyopo inatambuliwa kama janga ambalo linatishia kugharimu idadi kubwa ya maisha ya binadamu.
Ameeleza kuwa inakadiriwa kuwa kama hatua madhubuti hazitachukiwa janga hili litaua watu milioni 10 kwa mwaka ifikapo 2050.
Amesema kuwa tathmini iliyofanyika mwaka 2019 anaonesha uwepo na vifo vya watu takribani milioni 1.27, ambavyo vilisababishwa moja kwa moja na vimelea sugu kwa dawa, ambapo hivyo vifo vingi zaidi ya waliokufa kwa VVU au malaria.
Ameeleza kuwa serikali inatambua juhudi na misaada mbalimbali ya Kitaalam na Kifedha katika utekelezaji wa shughuli zote za mapambano ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa.
“Kipekee kabisa napenda kuwashukuru wanataaluma wote nchini, wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya afya, mifugo na kilimo na kamati ya kuu ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa (AMR), serikali ya Sweden kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa Sida pamoja na MUHAS” amesema.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala, Fedha na Mipango, Prof. Erasto Mbugi, amesema kuwa lengo kuu la Kongamano la kumi ni kukutanisha wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya usugu wa vimelea vya dawa nchini ikiwemo watunga sera, watumishi wa sekta ya Afya, watafiti, wanataaluma na washiriki wenza wanaosaidia kutekeleza shughuli zinazohusisha kupambana na janga hilo.
Prof. Mbugi amesema kuwa katika kongamano hilo matokeo ya tafiti za kisayansi yatawasilishwa na kujadiliwa kwa kina na kwa pamoja kupendekeza njia bora zaidi za kupambana na janga hilo la usugu wa vimelea vya dawa.
Amesema kuwa MUHAS ni moja ya taasisi inayoongoza barani Afrika katika mafunzo, ushauri na utafiti katika kukuza ubora na imejipanga kusaidia serikali katika kushughulikia tatizo la vimelea vya usugu wa dawa.
“Kongamano hili la siku moja limeandaliwa kimakusudi ili kutoa usaidizi kwa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kupambana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa (NAP -AMR 2023-2028) uliozinduliwa hivi karibuni, hivyo basi, mada zitakazojadiliwa zinaendana na malengo ya mpango kazi wa kitaifa na zinalenga kukabiliana na changamoto zinazotokana na vimelea sugu vya dawa nchini” amesema Prof. Mbugi.
Katika Kongamano la kumi la Kisayansi kauli mbiu “MAPAMBANO DHIDI YA USUGU WA VIMELEA KWA DAWA”