Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya maendeleo ya ushirika TCDC Dkt. Benson Ndiege, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika kwa maafisa ushirika kanda ya Morogoro May 17, 2023.
Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Mussa Ally Mussa akizungumza wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika kwa maafisa ushirika kanda ya Morogoro May 17, 2023.
Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Mussa Ally Mussa ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa wafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika kwa maafisa ushirika kanda ya Morogoro May 17, 2023.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Hussein Mohamed, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika kwa maafisa ushirika kanda ya Morogoro May 17, 2023.
…
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Serikali imeiagiza tume ya maendeleo ya ushirika (TCDC) kuhakikisha wanaongeza nguvu katika matumizi ya TEHEMA na kuwajengaea uwezo maafisa ushirika ili kuongeza ufanisi katika uzarishaji wa mazao na kujiimarisha kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika kwa maafisa ushirika kanda ya Morogoro na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Mussa Ally Mussa .
Amesema ili vyama vya ushirika viweze kujiendesha kwa faida niwazi kwamba suala la TEHEMA linatakiwa kuwekewa mkazo ili kuweza kuwahudumia watanzania hasa wakulima na kuondoa dosari zilizokuwepo hapo awali pamoja na kupunguza hoja kikaguzi katika vyama vya ushirika.
Amesema moja ya changamoto kubwa kwa katika vyama vya ushirika ni kukosekana maadili na uadilifu hali inayozorotesha utendaji kazi na kushindwa kuwahudumia wananchi.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa ukaribu na Mamlaka ya serikali za mitaa ili kuboresha maisha ya wananchi na kumaliza migogoro katika vyama vya ushirika hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji wenye tija.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Hussein Mohamed, amesema ili kufikia malengo ya serikali kupitia sekta ya kilimo kuchangia fedha za kigeni Bil. 5 na ajira kwa wananchi hasa vijana Bil. 3 ifikapo 2030 ni lazima kuwe na ushirika ulio bora.
Amesema ushirika unasaidia kuzalisha mazao yenye tija kwani upatikaji wa pembejeo ( Mbolea) kwa urahisi zaidi, kupata mikopo ya riba nafuu pamoja na kufikia masoko ya kimataifa.
Naye Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya maendeleo ya ushirika TCDC Dkt. Benson Ndiege amesema katika mwaka 2021hadi 2023, ziadi ya tani Bil. 1.092 za mazao ya kimkakati ya Tumbaku, Kakao, Pamba, Chai, Soya, Choroko, Korosho, Kahawa, Mkonge, na Dengu zimeuzwa kupitia Vyama vya Ushirika na Shilingi 2.9 zililipwa kwa Wakulima.
Pia katika Mwaka 2021/2022, Pembejeo za Kilimo zenye thamani ya jumla ya Sh. 397.7 zilinunuliwa kupitia Mfumo wa Ushirika hivyo kufanya wanaushirika kulima kilimo chenye tija.
Katika Kanda ya Morogoro mafunzo hayo yametolewa kwa washiriki sabini na nane (78) kutoka katika Mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar es Salaam na baadhi ya Maafisa kutoka TCDC Makao Makuu Dodoma.