Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Tunguu Mhe. Khalifa Salum Suleiman (mwenye baragashia) aliyeambatana na madiwani kutoka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar walipotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Mei 17, 2023 kwa lengo la kupata uzoefu katika masuala ya hifadhi ya mazingira. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi (mwenye miwani).
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Tunguu Mhe. Khalifa Salum Suleiman aliyeambatana na madiwani kutoka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar walipotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma kwa lengo la kupata uzoefu katika masuala ya hifadhi ya mazingira, leo Mei 17, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Tunguu Mhe. Khalifa Salum Suleiman (kulia kwake) aliyeambatana na madiwani kutoka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar walipotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma kwa lengo la kupata uzoefu katika masuala ya hifadhi ya mazingira, leo Mei 17, 2023. Kushoto kwa Waziri Jafo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi (kushoto).(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)