Waziri wa Nishati January Makamba (kushoto) akiongoza kikao kati ya Balozi wa Indonesia nchini Tanzania,Tri Yogo Jotmikob (wa pili kushoto) na Viongozi Waandamizi wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Pertamina ya nchini Indonesia, akiwemo Rais wa Kampuni hiyo John Anis (wa tatu kushoto) kuhusu kuongezewa hisa kwa kampuni ya Maurel & Prom katika Kitalu cha kuzalisha Gesi asilia cha Mnazi Bay mkoani Mtwara yaliyofanyika Mei 16, 2023 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati January Makamba (tatu kulia) katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania,Tri Yogo Jotmiko(wa pili kulia) Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji katika sekta ya Mafuta na Gesi ya Pertamina ya nchini Indonesia, John Anis (kulia), Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Macocha Tembele,( tatu kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame( wa pili kushoto) baada ya kumaliza kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizoko jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati January Makamba (kushoto)akimsikiliza Balozi wa Indonesia nchini Tanzania,Tri Yogo Jotmiko(katikati) na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Pertamina ya nchini Indonesia, John Anis (kushoto) wakati wa kikao kuhusu nia ya kampuni ya Maurel & Prom kununua hisa za mbia mwenza Wentworth resources katika Kitalu cha kuzalisha Gesi Asilia cha Mnazi Bay mkoani Mtwara kilichofanyika Mei 16, 2023 jijini Dar es Salaam.
….
Na Zuena Msuya DSM,
Waziri wa Nishati January Makamba amefanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania,Tri Yogo Jotmiko na Viongozi Waandamizi wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Pertamina ya nchini Indonesia akiwemo Rais wa Kampuni hiyo John Anis.
Mazungumzo hayo yamefanyika Mei 16, 2023 jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kuzungumzia suala la kampuni ya Maurel & Prom ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Pertamina kwa asilimia 100 kununua hisa za Kampuni ya Wentworth Resources ambaye ni mbia katika Kitalu cha Mnazi Bay mkoani Mtwara.
Makamba ameileza Kampuni hiyo kuwa Tanzania imeweka mazingira rafiki katika suala zima la uwekezaji hivyo kuhusu maombi yao, ameelekeza Taasisi husika ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu (PURA) kutakutana kwa pamoja ili kutazama suala hilo na kuishauri Serikali kama Sheria inavyoelekeza.
Viongozi wengine walioshiriki katika Kikao ni Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Macocha Tembele, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame na Viongozi wengine wandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu (PURA).
Kampuni ya Maurel & Prom imeonesha nia ya kununua hisa za Wentworth Resources ambaye ni mbia mwenza kwenye kitalu cha Mnazi Bay. Ununuzi huo utapelekea mabadiliko katika uendeshaji wa kitalu hicho (change of control) na kuongeza hisa za Maurel & Prom kutoka 48% za sasa hadi 80%, mbia mwingine katika kitalu hiki ni TPDC mwenye asilimia 20 ya hisa.