Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma tayari amewasili nchini Afrika Kusini na kupokelewa na baadhi ya Watanzania waishio nchini hapo kwa ajili ya kuongoza mashabiki wa Klabu ya Yanga kuishangilia timu hiyo, inayotarajiwa kushuka dimbani kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kesho Mei 17, 2023 dhidi ya Marumo Gallants ikiwa ni kuunga mkono timu hiyo katika katika jitihada zao za kuisaka Fainali.
Akizungumza baada ya kuwasili nchini Afrika Kusini, Mhe. Mwinjuma amesema Serikali haitaishia kukabidhi Bendera na kuwapokea washindi tu bali itaendelea kuwa na wawakilishi mbalimbali wa nchi kwenye michezo mbalimbali hatua kwa hatua wakati wote watakapokuwa wanaiwakilisha nchi.
Mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam Yanga iliibuka na Ushindi wa goli 2-0