Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Bw. David Kafulila leo tarehe 6 Mei alipokuwa anaongea na wahariri wa vyombo vya habari.
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuwakaribisha wawekezaji na kuendelea kuwasikiliza kero zinazowakabili ikiwa kwenye uwekezaji ikiwa ni kutambua mchango wako katika kuendeleza na kuleta maendeleo hapa nchini.
Haya yamesemwa leo na Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Bw. David Kafulila kwenye kikao na Wahariri ikiwa ni kueleza na kujenga uelewa juu ya majukumu yanayofanywa na idara hiyo leo tarehe 16 Mei ameongeza kwamba sheria za uwekezaji ni rafiki na kila mwekezaji anaruhusiwa kuleta andiko lake la kuwekeza sehem au kwenye mradi ambao ataridhika nao na tayari ofisi yake ina Maandiko mbali mbali kutoka kwa wawekezaji wanaomba kuwekeza hapa nchini huku akitolea mfano uwekezaji wa barabara nane za kibaha Chalinze ambao utagharimu Bilion mia nane(800) akieleza kwamba tayari kampuni kumi na tatu tayari zimekwisha peleka andiko na wanaendelea kuchambua ikiwa ni kutafuta kampuni yenye vigezo vya zaidi waweze kupewa tenda hiyo huku akisema baada ya ujenzi huo kampuni husika itakusanya ushuru kwa makubaliano watakayowekeana na serikali na kwamba ujenzi huo serikali haitagharamia hata shilingi moja gharama zote zitafanywa na kampuni husika.
Aidha ameeleza kwamba sekta hiyo inatoa na kusimamia mikataba yenye ubia kati ya Serikali na sekta binafsi, akieleza fursa nyingi kwa wawekezaji ikiwa pia mikataba ya wazi na mikataba yao ni ya muda mrefu kuazia mia ishirini(20) hadi miaka arobaini(40).
Kafulila Amesema Mikakati ya sekta hiyo ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo mbalimbali ya habari, majarida na mitandao ya kijamii ili waweze kupata wawekezaji wengi kwa nia na tija ya kuleta maendeleo hapa nchini huku akiwahasa wahariri kutumia vyombo vyao na nafasi zao kushawishi wawekezaji kujitokeza.
Kuhusu ujenzi wa Daraja lenye kilometa 38 kutoka posta hadi Zanzibar ameeleza kwamba tayari kuna kampuni kutoka China ambayo imekwisha leta andiko lake la kuhitaji kuwekeza kwenye ujenzi huo na tayari wapo kwenye mazungumzo.
Ameongeza kwamba serikali kupitia sekta binafsi zinatambua mwekezaji awe mkubwa ama mdogo mchango wao ni muhimu katika pato la taifa lakini pia makundi maalum ushiriki wao unatambulika.
Tanzania pia inatambua na kuzifuata sheria za kimataifa zinazohusiana na usimamizi wa sheria za Biashara na uwekezaji ulimwenguni hivyo kuwatoa hofu wawekezaji kutoka mataifa ya mbali wenye nia ya kuja hapa nchini kuwekeza.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania ndugu Deodatus Balile amemshukuru kamishina wa PPP kwa kutoa elimu kwa wahariri na kuwaelekeza mikakati ya sekta hiyo huku akimuhaidi kwamba jukwaa hilo litashirikiana naye kwenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi na wawekezaji kwa ujumla kupitia vyombo vyao vya habari.