Mei, 15, 2023 Askari wa TAWA Kanda kati walifanikiwa kumdhibiti chatu aliezua taharuki Kwa wakazi wa Kijiji Cha Matomongoli, kata ya Mkoka, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Chatu huyo aliyekuwa amemeza mbuzi alizua taharuki kubwa Kwa wananchi kiasi Cha kupelekea kutoa taarifa Ofisi za TAWA Kanda ya kati Ili kuomba msaada ambapo mara moja wataalamu wa Nyoka walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumdhibiti mnyama huyo Kwa kumhamisha eneo hilo na hatimaye kumpeleka sehemu salama mbali na makazi ya watu.
Hii ni mojawapo ya jitihada za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) katika kuhakikisha inapunguza adha wanayoipata wananchi kutokana na Wanyamapori ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti kabla hawajaleta madhara Kwa binadamu