Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefika katika Soko la Kariakoo ambako wafanyabiashara wametangaza mgomo tangu asubuhi.
Kwa mujibu wa Majaliwa amelazimika kuacha Bunge na kuja kwa dharura ili kuzungumza na wafanyabishara hao kwa lengo la kupata suluhu.
Awali taarifa kutoka ofisi yake ilisema kuwa kiongozi hiyo angekutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko hilo keshokutwa Jumatano Mei 17, 2023.
Katika mkutano huo Waziri Mkuu Majaliwa alipanga kukutana pia na mawaziri wa sekta hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye ofisi yake Magogoni-Ikulu na kuratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.
Hata hivyo, wafanyabiashara hao hawakusitisha mgomo huo na kudai kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan.