Na Ahmed Mahmoud
Serikali inaamini kuwa siku ya Familia Duniani ni siku muhimu Sana ya kukumbusha na kuhimiza jamii kujenga upendo na umuhimu wa makuzi ya watoto nchini sanjari na Kutoa elimu Kwa jamii Ili kupunguza ukatili wa kijinsia.
Tumepiga kelele na Serikali imetoa waraka hakuna kumpeleka mtoto Shule za Bweni Kutoka awali hadi darasa la nne hivyo tunazidi kupiga kelele zaidi Ili angalau kidato Cha kwanza ndio Mtoto aende shule za Bweni.Sasa Hivi tunapiga marufuku mabasi kuonyesha picha za vita Kwani misingi ya watoto inaanzia hapo kuharibika
Rai hiyo imetolewa kwenye Maadhimisho ya siku ya Familia (Mother Day) Jijini Arusha iliyoandaliwa na Taasisi ya Husna Foundation Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha Blandina Nkini ambapo Amesema jamii inahitaji kuimarisha upendo Kwa familia Ili kukuza maadili.
Alisema kuwa miongoni mwa jamii makuzi na malezi yamezidi kuporomoka ikiwemo ndoa kuvunjika jambo linalopelekea familia na watoto kukosa upendo hivyo kuwaa bila maadili na ufuatiliaji wa baba na Mama.
“Niwaombe Sana elimu hii mnayopata mkawe mabalozi Wazuri wakuifikisha Kwa jamii Ili kuondokana na ombwe la kuporomoka Kwa maadili nchini sanjari na vitendo vya ukatili wa kijinsia kama Serikali inaungana na Taasisi hii kuhimiza wazazi na jamii kulinda maadili na kupiga vita suala la mapenzi ya jinsia moja”
Kwa Upande wake Mkuu wa Dawati la jinsia Mkoa wa Arusha la Jeshi la polisi Happyness Temu Amesema kwamba matukio ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto yamekuwa yakiripotiwa Sana hii inaonyesha maadili ya makuzi Kwa watoto wetu hayapewi umuhimu unaostahili.
Amesema Jeshi Hilo litaendelea kuhimiza juu ya makuzi na maadili Kwa jamii Kwani upigaji vita unahitaji ushirikiano wa Jamii na sio suala la Jeshi Hilo pekee hivyo Kutoa wito Kwa wananchi kuisaidia kusimamia suala Zima la malezi Kwa watoto wetu.
“Niwaombe washiriki wenzangu Ili kumpatia Upendo na malezi kijana wazazi lazima tuanze kushirikiana kufuatilia mwenendo wa Watoto wetu kama baba na Mama ili kumkuza kijana na maadili mema hii itapelekea kuzuia Masuala ya mazima ya ukatili wa jinsia.”
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Husna Foundation Husna Alma’s Amesema kwamba Pamoja na Taasisi hiyo kujikita Kutoa elimu mashuleni vyuoni na mitaani Bado wanakwbiliwa na upungufu wa vifaa Ofisi na kuomba wadau mbalimbali wa Maendeleo kujitokeza kusaidiana nao.
Amesema kwamba Taasisi hiyo mbali na mafanikio kadhaa Imekuwa pia ikishirikiana na wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kuwafikia wananchi na baada ya kuanza safari hiyo Kwa mkoa wa Arusha wataendelea Kwa mikoa mingine hapa nchini.
Niwaombe Taasisi hii imeanzishwa miaka 3 iliyopita ikiwa na lengo la kusaidia vijana wagame wajane wazee na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hivyo wadau wa Maendeleo waendelee kutuunga mkono Ili kufikia jamii yote hapa nchini.