OR TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deo J. Ndejembi amesema Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya michezo katika shule teule 56 nchini ikiwa ni wastani wa shule mbili kwa kila Mkoa.
Ameeleza hayo Bungeni Dodoma wakati alijibu Swali la Mhe. Anastazia James Wambura, Mbunge wa Viti Maalum, aliyetaka kujua Je, lini Shule ya Sekondari Mkalapa itatambuliwa kuwa Shule ya vipaji vya michezo ya mpira wa wavu.
Ndejembi amesema Serikali inapokea ombi la Mheshimiwa Mbunge la kuitambua shule ya Sekondari Mkalapa kuwa shule ya vipaji vya mchezo wa wavu.
Aidha, amewaelekeza wataalamu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kutembelea shule hiyo ili kuona miundombinu iliyopo na namna shughuli za michezo zinazofanyika shuleni hapo ili kuona kama inakidhi vigezo vinavyotakiwa.
Ndejembi amesema Serikali kupitia ajira mpya zilitangazwa itahakikisha inatoa fursa kwa Waalimu wa Michezo, Kilimo na walimu wa ufundi ili kuboresha utoaji wa elimu nchini.