Baadhi ya wahitimu wa Chuo Cha Furahika wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Khalid Mbaruku pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Furahika Dkt. David Msuya.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Khalid Mbaruku ambaye ni mgeni rasmi wa Mahafali ya Chuo Cha Furahika akizungumza na wahitimu wa Chuo hicho leo tarehe 13/5/2023 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Furahika Dkt. David Msuya akizungumza na wahitimu katika Mahafali yaliofanyika Leo tarehe 13/5/2023 jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa wahitimu wa Chuo Cha Furahika waliofanya vizuri katika masomo yao akipewa mkono wa pongezi na Mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Khalid Mbaruku.
Baadhi ya wahitimu pamoja na wazazi wakiwa katika Mahafali ya Chuo Cha Furahika.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wahitimu 200 wa Chuo Cha Furahika kilichopo Buguruni Jijini Dar es Salaam wametakiwa kuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kufanya kazi kwa bidii jambo ambalo litasaidia kufikia malengo tarajiwa katika familia na Taifa.
Akizungumza leo tarehe 13/5/2023 katika Mahafali ya Chuo Cha Furahika, Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Khalid Mbaruku, amesema kuwa jamii inapaswa kuwa wazalendo pamoja na kufanya kazi wa uweledi ili kuleta tija kwa Taifa.
Bw. Mbaruku ni mgeni rasmi katika Mahafali haya, amesema kuwa wahitimu wanapaswa kuendelea kusoma kutokana Taifa bado linaitaji wasomi wengi ili liweze kuendelea.
“Tukiwa na wasomi wengi ikiwemo madaktari na wanasayansi tutamsaidia Rais wetu aweze kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali na kufikia malengo tarajiwa” amesema Bw. Mbaruku.
Amefafanua kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani amekuwa akitoa fursa ya mikopo isiyokuwa na riba kwa vijana kwa ajili ya kuhakikisha wanapiga hatua katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi.
Amesema kuwa Mhe. Dkt. Samia pamoja na serikali yake inafanya kazi kubwa katika kutekeleza ilani ya CCM kila sehemu, hivyo vijana wana uwajibu wa kusema mazuri yanayofanywa na Rais.
“Tukiwa majumbani tuseme mazuri ambayo anafanya Rais wetu, tunatakiwa kuwa na maadili, kwani kijana ni Taifa la leo na kesho, tuishi katika mila na desturi za kitanzania pamoja na kupinga matumizi ya dawa za kulevya” amesema Bw. Mbaruku.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Furahika, Dkt. David Msuya, amesema kuwa Chuo kupitia wafadhili wamekuwa wakitoa elimu bure kwa lengo la kuunga juhudi zinazofanywa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani.
Dkt. Msuya amesema kuwa wanafunzi wamekuwa wakichangia Sh 50,000 kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia kwa vitendo na kukifanya Chuo kuwa kimbilio kwa vijana ambao hawakufanya vizuri katika masomo ya kidato Cha nne pamoja na familia masikini ambazo hazina uwezo wa kuwasomesha watoto wao.
Amesema kuwa kila mwaka Chuo Cha Furahika kinatoa fursa ya kupokea wanafunzi 200 kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kusoma bure kozi ambayo ameichangua.
“Ni Chuo bora kwa sababu kuna kila kitu ikiwemo hosteli, pia Chuo kinashirikiana na serikali kupitia Wizara ya Elimu katika kuleta wanafunzi” amesema Dkt. Msuya.
Dkt. Msuya amebainisha kuwa tayari wamefungua dirisha la maombi ya kujiunga na Chuo ambalo linatarajiwa kufungwa mwezi mei mwaka huu.
Muhitimu wa Chuo Cha Furahika Kozi ya Cleaning and Forward, Bi. Tabu Gambi, ameishukuru uongozi wa Chuo kwa ushirikiano ambao wameutoa katika kumpatia elimu ambayo ni msaada mkubwa katika maisha yake.
“Nitakuwa balozi mzuri wa Chuo itakapokwenda kwa kufanya kazi wa bidii na juhudi ili kuhakikisha nafanikisha malengo yangu” amesema Bi. Gambi.
Chuo Cha Furahika kinatoa kozi mbalimbali ikiwemo Computer Application, Computer IT, Ufundi wa kushona, Ufundi wa magari, Ufundi umeme, Cleaning and Forward, Secretary Course, Hotel Management, Mapambo Ususi pamoja na Ukataji wa maua.