NJOMBE.
Katika jitihada za kulinda na kutetea haki za raia ,waandishi wa habari mkoani Njombe wametakiwa kutumia weledi na taaluma yao kuandika habari ambazo zitasaidia kudhibiti matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanaume,watoto na wanawake ambao unashika kasi hivi Sasa mkoani humo.
….
Katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyokuwa yafanyike Mei 3 na mkoa wa Njombe kuamua kuadhimisha Mei 13 mkuu wa dawati la jinsia mkoani humo Wilfred Willa amesema vyombo vya habari vinapaswa kutumia weledi na kuzingatia miiko na maadili katika kazi yao kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikijitokeza kila uchwao na kuathiri wahanga kwa kiasi kikubwa.
Mbali na Hilo Willa ametaka waandishi wa habari kuwa waelewa Pindi wanapoambiwa na mamlaka mbalimbali wasubiri kupata mizania hususani kwa taarifa zinazohusu jeshi la Polisi kwasababu wanaochapisha ama kurusha taarifa ambazo hazijakamilika wanaweza kuharibu uchunguzi na kukimbiza wahalifu.
Awali akifungua maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amesema kuanzishwa kwa siku hiyo Kuna faida kubwa sekta ya habari kwasababu wanahabari wanatumia kutathimini wametoka wapi,wanaenda wapi na Hali ikoje na Kisha kuja na muarobaini wa vikwanzo vyao.
Kuhusu changamoto zinazokikabili chama Mpete amesema atatumia nafasi yake kusaidia wanahabari kupata eneo la ujenzi wa ofisi za chama na shamba la parachichi huku akisema ili kupata vitu hivyo chama kiandike barua kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri mji wa Njombe kuomba kiwanja na shamba .
Suala la sheria kandamizi Mwenyekiti huyo wa halmashauri amesema serikali inaendelea kufanya marekebisho ya sheria hususani ya huduma za habari ili kutoa Uhuru kwa wanahabari kufanya kazi yao bila kukwamishwa na chochote
Amesema tayari Rais amefanya mabadiriko makubwa katika kuboresha Uhuru wa habari ambapo amesema wote tumeona vyombo vilivyofungiwa vimefunguliwa na waandishi waliokamatwa kuachwa huru .
Katika hatua nyingine ametaka waandishi kutumia vyombo vyao kuandika kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Njombe ikiwemo ya Liganga na mchuchuma wilayani Ludewa.
Nae Mdau wa habari Johnson Mgimba ametoa maoni yake kuhusu Hali ya Uhuru wa vyombo vya habari kwasasa nchini ukilinganishwa na miaka mitatu iliyopita ambapo amesema rais Samia amefanya Jambo kubwa kupunguza tozo za usajili vyombo vya habari mitandaoni kwani vijana wengi wanajiajiri Huko.
Kwa upande wake Emmanuel Kalemba na Tatu Abdallah ambao ni waandishi wa habari wameeleza namna baadhi ya maofisa wa serikali wanavyochangia wanahabari kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa kitendo Cha kuchelewa kutoa taarifa Pindi wanapohitaji kufanya mizania ya taarifa zao.
Damiani Kunambi Mwenyekiti wa chama Cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC amesema ili tasnia ipate ustawi ni lazima baadhi ya sheria kandamizi ziondolewe ama kuboreshwa huku pia akitaka maslahi kwaandishi yaboreshwe.
Mwakilishi wa wamiliki wa vyombo vya habari mkoani Njombe ambaye ni Mkurugenzi wa Uplands fm Humphrey Milinga amekumbusha wanahabari kufanya kazi kwa bidii ili wapate maslahi mazuri na Kisha kuhimiza kuacha tabia ya kuandika zaidi habari za majukwaani na badala yake wafanye uchunguzi ili kusaidia taifa.