Na Mwandishi Wetu, Los Angeles, California
Moja ya kampuni kubwa duniani miongoni mwa zinazosimamia watu mashuhuri (celebrity management) ya jijini hapa, Creative Artists Agency (CAA), iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kutumia watu mashuhuri kutangaza utalii.
Akizungumza jana na Katibu Mkuu-Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, kwenye makao makuu ya CAA, Beverly Hills, mjini hapa, Meneja wa Divisheni ya kusimamia baadhi ya wasanii mashuhuri, Bw. Ozi Menakaya, ameeleza kuwa kampuni hiyo inasimamia watu mbalimbali mashuhuri wawe wa michezo, sanaa, filamu na fani nyingine mbalimbali.
“Watu mashuhuri wana nafasi kubwa ya kuitangaza nchi na hasa utalii wake, CAA iko tayari kushirikiana na Tanzania kwa kuwaunganisha ninyi na wateja wetu mashuhuri zaidi ya 3,000,” alisema.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali CAA inashika nafasi ya kwanza au wakati fulani kuwa katika tatu bora kwa ukubwa katika kusimamia watz mashuhuri duniani.
Miongoni mwa mastaa wanaosimamiwa na kampuni hiyo ni nyota wa filamu ya “The Lion King” na mwimbaji wa singo mashuhuri ya “Irreplaceable”, Beyonce; staa wa filamu za “Bad Boys” na “Men in Black”, Will Smith; na mwanamuziki wa hip-hop ambaye pia ni mwenza wa staa mwingine wa muziki, Rihanna, ASAP Rocky.
Baadhi ya mastaa wengine chini ya usimamizi CAA ni: Maria Carey, Babyface, Morgan Freeman, Boyz II Men, Ciara, Eve, Faith Evans, Janeth Jackson na wengine wengi. Tembelea: