Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amewataka madiwani Pamoja na watendaji wa serikali kushirikiana kwa pamoja pasipo kuwekeana vikwazo kwani endapo wataonyesha ushirikiano kati yao itasaidia kuleta maendeleo kwa haraka.
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo katikati kikao cha Baraza la madiwani ambacho ni kikao chake cha kwanza kushiriki toka kuteuliwa kwake na kuongeza kuwa madiwani wana haki ya kushirikishwa katika mambo ya maendeleo yoyote yanayopelekwa katika kata yake ili waweze kuufahamu vyema na kuusemea kwa wananchi.
Amesema kumekuwa na mazoea kwa baadhi ya wataalam kukumbatia taarifa za miradi pamoja na fedha za kata fulani pasipo diwani wa kata husika kushirikishwa kitu ambacho si sahihi kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi na wamechaguliwa na wananchi hao kwaajili ya kuwasemea changamoto zao na kupeleka mrejesho wa maendeleo yaliyofika ndani ya kata”
“Hawa madiwani wakipewa taarifa na kuelimishwa vyema juu ya maendeleo na miradi inayokuja katani mwao ni rahisi kuwashirikisha wananchi nao wakashiriki kwa namna moja ama nyingine”