Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Masoud Suleiman Makame akizungumza wakati alipokua Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar,huko Ofisini kwake Maisara Mjini Unguja.
…
Na Rahima Mohamed – Maelezo
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukuwa juhudi mbalimbali zikiwemo kuhamisha data zilizochukuliwa katika maeneo ya Zanzibar kutoka Taasisi za Tanzania Bara ili kuendeleza shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Masoud Suleiman Makame wakati akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara Mjini Zanzibar.
Amesema data hizo ni muhimu katika utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia ambazo zimechukuliwa nyakati tofauti katika eneo la bahari ya Mashariki mwa Zanzibar na kitalu kinachoitwa Pemba Zanzibar Block.
Aidha amesema Wizara ya Uchumi wa Buluu kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia imesaini mkataba na Kampuni ya Kimataifa ya Schlumberger ili kuzitafsiri data hizo na kufanya tathmini ya maeneo yenye viashiria vya uwepo wa rasilimali hizo.
Vilevile amesema mkataba huo utawajengea uwezo watendaji wa Taasisi ya Mafuta na Gesi Asilia ,kukata vitalu vipya,pamoja na kuzitangaza data za Zanzibar katika majukwaa ya kitaifa ili kuweza kuwavutia wawekezaji wakubwa wa sekta ya mafuta na gesi asilia.
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa shilingi milioni 700 za Kitanzania kwa ajili ya kuanza mchakato wa ujenzi wa kituo cha Taifa cha Data za Mafuta Zanzibar ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.

Hata hivyo amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeanza na utaratibu wa kulifungua eneo la Pemba –Zanzibar kwa uwekezaji mpya wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta gesi asilia.
Waziri Masoud amesema Serikali ikishirikiana na Kampuni ya RAKGAS inaendelea na zaoezi la ulipaji fidia wananchi walioathirika na zoezi hilo kwa njia ya mtetemo.
“Jumla ya madai 4,306 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.39 yalisajiliwa kwa Unguja na Pemba ambapo hadi sasa madai ya2,587 tayari yameshalipwa yenye thamani ya Bilioni 1.09 TZS”Alisema Waziri huyo.
Aidha amesema katika ulipaji wa fidia hizo changamoto mbalimbali zilijitokeza ikiwemo waliohakikiwa kurudia tena kudai,kutojaza fomu kikamilifu pamoja na wananchi kutoenda kufata fedha zao baada ya kukabidhiwa vocha za malipo.Hivyo aliwataka wananchi waliohakikiwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha zoezi hilo.