…………………….
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Shule ya msingi Njiwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayowalazima wanafunzi 172 kutumia chumba kimoja cha Darasa.
Shule hiyo inavyumba 10 pekee wakati uhitaji ni wastani wa vyumba 37 kuwezesha wanafunzi 1718 wa shule hiyo kukaa kwa uwiano unaokubalika
Afisa elimu taaluma Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Fatuma Abdallah akisoma taarifa mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 Abdulla Shaib Kaim,amesema Katika kuwasaidia wanafunzi waweze kusoma kwenye Mazingira rafiki wakazi wa kata ya Itete Njiwa walikubaliana kujiyolea michango na nguvukazi na kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na Ofisi.
Shule ya msingi Njiwa ni miongoni mwa shule za Muda mrefu, pamoja na kuwa miundombinu yake hasa madarasa yanayotumika kuwa chakavu, pia imeonekana kuelemewa kwani kuna vyumba vya madarasa 10 pekee kati ya 37 vinavyo hitajika kuwezesha wanafunzi 1718 waliopo kukaa Kwa uwiano.
Kwa Upande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim amesisitiza kuimarisha usimamizi kwenye utekelezaji wa Miradi ya maendeleo pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma.
Mbunge Jimbo la Malinyi Antipas Mgungusi ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kupeleka Fedha kwenye Jimbo lake na kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali.
Pamoja na mradi huo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na Ofisi shule ya msingi Njiwa, Katika wilaya ya Malinyi Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umefikia jumla ya Miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 800.