Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-
1. Amemteua Prof. Elifas Tozo Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Prof. Bisanda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa kipindi cha pili.
2. Amemteua Mhandisi Abdallah Mohamed Mkufunzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maji. Uteuzi wa Wenyeviti hao umeanza tarehe 05 Mei, 2023.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu