Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Namibia (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek, mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano wa Kimtaifa wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah, wakati Rais Samia alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi Maalum kutoka kwa Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023, wakati Rais Samia alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.