Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure (kushoto) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa –RAS, akizindua rasmi ripoti ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni. Wanaoshiriki ni Mkurugenzi Mtendaji wa Organization for Community Development (OCODE), Joseph Jackson (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati za Shule zilizo chini ya Miradi ya OCODE, Bw. Hamza Mirambo. |
Mratibu wa Tathmini wa Stadi za Maisha na Maadili (ALiVE) Wilaya ya Kinondoni, Bi. Tunu Sanga akisisitiza jambo katika hafla hiyo. |
Mmoja wa vijana wanufaika na miradi ya OCODE akielezea namna ilivyomnufaisha. |
Mdhibiti Mkuu Ubora wa Shule Kinondoni, Bi. Naitwa Mgumba akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya ALiVE Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam. |
Kinondoni imezinduliwa rasmi na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa –RAS.
ripoti hiyo ya kupima tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) ya
vijana umefanyika katika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na washiriki katika hafla ya uzinduzi wa matokeo ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, aliitaka jamii kubadilika katika mtizamo wa malezi ndani ya familia.
Alisema ipo haja ya kuanza kuwaandaa vijana wetu kuanzia ngazi ya familia, kwa sababu vijana wanaanza kujifunza maadili kuanzia ngazi ya familia.
”…Mfano mzuri wa baadhi ya wazazi kujisahau katika kuwajenga vijana
unaweza kukuta mzazi anaona taa imesahaulika inawaka bila matumizi sahihi mzazi badala ya kumwambia mtoto wake akazime taa hiyo anamuita binti wa kazi ndio
anampa maelekezo ya kuzima taa hiyo, sasa huku ni kujisahau kimalezi katika kuwajenga vijana kuanzia ngazi ya familia…,kimsingi mzazi unapaswa kuanza kumwambia mtoto wako kwanza,” alisema Bi. Sure.
Alisema tunu za maadili na kujielewa kwa vijana inapaswa kuanzia katika
ngazi ya familia na kupanda juu ili kuwaandaa vijana kujitambua.
Awali akisoma matokeo ya taarifa hiyo, Mratibu wa Tathmini wa Stadi za
Maisha na Maadili (ALiVE) Wilaya ya Kinondoni, Bi. Tunu Sanga alibainisha kuwa jumla ya vijana 363 wa kuanzia miaka 13 hadi 17 kutoka katika kaya 322
walifanyiwa tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) huku ikionesha ni vijana 6 kati ya 10 wenye uwezo wa kutatua matatizo yao.
Katika kujitambua na kujidhibiti ni vijana 6 kati ya 10 walionesha
kujitambua, na katika kujitambua na kimtizamo ni vijana 7 kati ya 10 walionesha kumudu hali hiyo. Aliongeza kuwa katika tunu ya heshima ni vijana 6 kati ya 10 ndio waliomudu tunu ya maadili.