Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kata Makuburi Bi. Severina Minga (kushoto) akimkabidhi ripoti ya utendaji Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Ubungo Bi. Samina Mashauri wakati akifanya ziara katika Kata hiyo kuangalia uhai wa Jumuiya.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kata ya Makuburi, Bi. Nuru mwaijande akizungumza jambo.
Diwani wa Viti Maalum na Mlezi wa Kata Makuburi UWT, Bi. Elga Elisha akizungumza na wanachama wa UWT namna alivyojipanga kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu ya UWT.
Wanachama wa UWT Kata ya Makuburi wakiwa katika mkutano wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Ubungo Bi. Samina Mashauri.
….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Ubungo Bi. Samina Mashauri ameipongeza UWT Kata ya Makuburi kwa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za Chama jambo ambalo limesaidia kuleta tija na kupiga hatua katika maendeleo.
Akizungumza leo tarehe 5/5/2023 jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara kwa ajili ya kuangalia uhai wa UWT Kata Makuburi Bi. Mashauri, amesema kuwa viongozi wamekuwa wakifanya kazi nzuri, huku akiwataka waongeze nguvu ya kushuka ngazi ya matawi kwa ajili kuhamasisha wanawake kujiunga na UWT.
“Wanawake wanapaswa kujiunge na Jumuiya yetu UWT pamoja na kuendelea kushawishi wananchi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwani kuna ilani nzuri inayotekeleza” amesema Bi. Mashauri.
Bi. Mashauri, amesema kuwa kutokana na changamoto zilizopo ikiwemo ukosefu wa Ofisi, anaendelea kulifanyia kazi ili kuangalia namna ya kutatua ikiwemo kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi, huku akiendelea kuwapongeza uwa na mkakati wa kukodi Ofisi ambayo wataitumia katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amewakumbusha wakinamama kuwa karibu na watoto kwani sasa hali ya maadili katika jamii sio rafiki hivyo wanapaswa hivyo tunapaswa kuendelea kutoa elimu pamoja na kukemea matendo maovu.
“Tusiwaamini sana ndugu zetu, tuendelee kuziombea familia zetu ili ziweze kuishi katika mazingira rafiki na Mwenyezi Mungu hatuepushe na tabia zenye madili mabovu” amesema Bi.Mashauri.
Mlezi wa Kata ya UWT, Diwani wa Viti Maalum, Bi. Elga Elisha, amesema kuwa ataendelea kuwasaidia katika kutatua changamoto zilizopo ikiwemo kuwasaidia kuanzia mradi wa Steshenary.
“Nitawasaidia kuwapa computer na printer kwa ajili ya kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ndani ya UWT Kata ya Makuburi” Bi. Elisha.
Amewakumbusha viongozi wa UWT Kata ya Makuburi kuwa na utamaduni wa kuwasilisha changamoto zao kwake kwa ajili ya kupatiwa majibu kwa maendeleo ya chama.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kata ya Makuburi, Bi. Nuru mwaijande, amesema kuwa lengo la ziara ya Mwenyekiti Bi. Mashauri kuangalia uhai wa Jumuiya pamoja kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo.
Bi. Mwaijande amesema kuwa wanawake wanapaswa kuwa na upendo na mshikamano pamoja na kushirikiana na serikali katika kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata ya Makuburi na Taifa.
“Tumeyapokea maagizo yote kwa ajili ya kuyafanyia kazi, tumejipanga kuhakikisha tunasaidiana kiuchumi na tupo tayari kwa utekelezaji maagizo muda wowote kutoka kwa viongozi wetu ikiwemo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani kwani wanawake ni Jeshi kubwa tunaweza” amesema Bi. Mwaijande.
Akisoma ripoti ya utendaji Katibu wa UWT Kata Makuburi Bi. Severina Minga, amesema kuna wanachama 2, 674 ambao tayari wamesajiliwa katika daftari, huku wakiendelea kuhamasisha ili kupata wanachama wapya UWT.
Bi. Minga amesema kuwa wanaendelea na utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Chama ili kuleta tija.
“Tunaendela kutafuta wanachama wapya, lakini tuna changamoto ya upatikanaji wa kadi za CCM na UWT na kusababisha zoezi la usajili wa electronic kusuhasua” amesema Bi. Minga.
Amefafanua kwa sasa wana mikakati ya kukodi ofisi kwa ajili ya shughuli za UWT pamoja kununua viti kwa ajili ya kukodisha ili kupata kipato.
Pia wana mpango wa kununua bajaji kwa ajili ya biashara ambapo mpaka sasa tayari wamekuchangisha Sh 400,000 ili kufanikisha malengo tarajiwa.