Na Dotto Mwaibale, Singida
WAMACHINGA
Mkoa wa Singida wameiomba Manispaa ya Singida kuanzisha mnada (GULIO) wa
kila Ijumaa mara ujenzi wa ofisi yao inayojengwa jirani na Uwanja wa Ndege Kata
ya Mandewmjini hapa kukamilika.
Ujenzi huo unafanyika baada ya Rais Dk.Samia
Suluhu Hassan kutoa Sh.Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo ya
wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga ambao kwa muda mrefu walikuwa
na changamoto ya kutokuwa na ofisi hivyo kushindwa kuwa na eneo lakuzungumzia
mambo yao ya biashara.
Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Singida, Ismail
Otta, alisema mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo wanaiomba
Manispaa ya Singida ianzishe mnada wa kila Ijumaaambao utasaidia kuwaleta
wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali na watu kupata mahitaji yao na
manispaa hiyokupata fedha kutokana na ushuru ambao utakuwa ukiipwa na
wafanyabiashara hao.
Alisema kwa muda mrefu changamoto yao kubwa
ilikuwa ni kutokuwa na ofisi jambo lililokuwa likisababisha wakose sehemu ya
kukutana na badala yake walipohitaji kufanya mkutano walipigiana siku na
kukutana maeneo tofauti tofauti hapa mchini.
Otta alitumia nafasi hiyo kumshukru Rais Samia
kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa alipokutana na wamachinga jijini Dodoma ambapo
aliahidi kutoa Sh.milioni 10 kwa kila mkoa kwa ajili ujenzi wa ofisi za
wamachinga jambo ambalo amelitekeleza.
Alisema katika Mkoa wa Singida kumekuwa hakuna
migogoro na mivutano ya wamachinga kutokana na ushirikiano mzuri wanaoupata
kutoka kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Jeshi
Lupembe, akizungumza wakati wa uzinduzi
wa ujenzi wa ofisi hizo ambao utagharimu Sh.Milioni 46 alisema ofisi hizo pia
zitatumiwa na madereva wa bajaji na bodaboda.
Alisema kutokana gharama hizo Halmashauri ya
Manispaa ya Singida itaongezea
Sh.milioni 36 na kwamba ili kuzifanya ofisi hizo zichangamke kila siku ya Ijumaa
ya kila wiki kutakuwa na gulio ambalo wafanyakazi watakuwa wakiuza bidhaa
mbalimbali kama walivyoomba wafanyabiashara hao.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi
Kiaratu, alimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha hizo na kumhakikishia kuwa
Manispaa itasimamia na kuongeza fedha za kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo
kupitia mapato yake ya ndani.
Alisema kujengwa kwa ofisi hizo kutakuwa na
manufaa kwa pande zote mbili kwani ofisi hizo zikitambulika itakuwa rahisi kwa
Manispaa au serikali itakapowahitaji viongozi wa wamachinga kuzungumza nao
jambo fulani kwa ajili ya maendeleo.
“Halmashauri ya Manispaa ya Singida Ina
lengo zuri kulifanya eneo hili kuwa mnada ambao utatoa fursa kila mtu kuleta
bidhaa zake mwenye kuchoma nyama atachoma,mwenye kuleta viatu au kinywa ataleta
na bodaboda wataweza kupata wateja kuwasafirisha,” alisema.
Kiaratu aliwataka watendaji kila mtu kusimamia
majumuku yake ili Halmashauri ya Manispaa ya Singida Singida iendelee kusonga
mbele na kuiga mfano wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Lupembe ambaye wakati wa
siku ya wafanyakazi Mei Mosi alitunukiwa tuzo kutokana na uchapa kazi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Jeshi Lupembe, akitoa taarifa wakati wa uzinduzi huo..
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida akishiriki kuchimba mtaro wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Hassan Mkata akishirikikuchimba msingi huo.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Hassan Mkata, akizungumzia ujenzi huo
Mmoja wa viongozi wa Wamachinga, Mkoa wa Singida, Asha Shabani akishiriki kuchimba msingi huo
Msingi ukichimbwa
Afisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Erick Simkwembea akizungumzia ujenzi wa ofisi hiyo
Mwenyekiti waWamachinga Mkoa wa Singida. Ismail Otta akizungumzia mambo mbalimbali kuhusu kazi zao na ujenzi wa ofisi hiyo
Mwenyekiti wa Bodaboda na Bajaj Mkoa wa Singida, Abdu Mitigo akizungumza.