Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla leo ameweka jiwe la msingi kwenye Jengo la Dharura kwenye Hospital ya Jeshi la Magereza Ukonga ambayo inatoa huduma za Afya kwa Jeshi la Magereza na Wananchi zaidi ya laki Tisa wa Jimbo la Ukonga.
Akizungumzia wakati wa Hafla hiyo, RC Makalla amemshukuru Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Shilingi Milioni 950 kwaajili ya ujenzi huo ambapo Shilingi Milioni 350 zimejenga majengo na Milioni 600 zimehusika kwenye Ununuzi wa Vifaa tiba.
Aidha CPA, Makalla amepongeza Jeshi la Magereza Kasi ya ujenzi ambapo mpaka Sasa hospital imekamilika kwa asilimia 95 huku wakiomba kuongezewa Shilingi Milioni 118 Ili ikamilike kwa asilimia 100 ambapo Mkuu wa Mkoa amepokea kwa mikono miwili ombi Hilo na Ameahidi kulifanyia kazi.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema uwekezaji jiwe la msingi wa jengo Hilo ni sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Muungano ambapo pia
Ametoa wito kwa Jeshi Hilo kuendelea kushirikiana na Wananchi wa Ukonga katika masuala mbalimbali ya kijamii.