John Walter-Arusha
Nchi za Afrika Mashariki zimetakiwa kuongeza fedha za bajeti ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula baina ya nchi hizo Wanachama ambazo zinakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na athari za ukame Pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wakizungumza katika Mkutano wa Sita wa Kisekta na bajeti ya Kilimo kwa nchi za Afrika Mashariki uliondaliwa na Esaff ,Mwenyekiti wa Mtandao wa Wakulima Afrika Mashariki na Kusini (ESAFF) Hakim Balirane amesema sasa ni muafaka wa nchi za Afrika kutenga fedha za kutosha kwenye bajeti ya kilimo ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa Malabo.Bajeti itasaidia kuboresha sekta ya kilimo na kuongeza upatikanaji wa chakula katika bara la Afrika linalokabiliwa na ukame Pamoja na njaa katika baadhi ya nchi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na Wafugaji Tanzania (MVIWATA) Apollo Chamwela amesema kuwa wakulima wanapaswa kuelimishwa juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi na kupewa mbinu za asili za kukabiliana na mabadiliko hayo ambazo haziharibu mazingira.
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Usalama wa Chakula Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Julius Mundia amesema kuwa jumuiya hiyo itaendelea kutunga sera na kanunizitazaoiwezeshe sekta ya kilimo kukua kwa kasi hususan katika Nyanja za pembejeo .