……………………
Mkurugenzi wa Idara ya Malikale nchini Dkt. Christowaja Ntandu leo tarehe 03 Mai 2023 Jijini Dodoma, amekutana na Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zikizokasimishwa vituo vya Malikale Kwa lengo la kupata uwelewa wa pamoja juu ya maboresho ya Ada mbalimbali kwenye maeneo ya Malikale nchini.
Taasisi zilizoudhuria kikao kazi hicho ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro – NCAA, Makumbusho ya Taifa – NMT, Hifadhi ya Taifa -TANAPA, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, Kitengo cha Sheria na Wataalam wa Idara ya Malikale .