…….
Na Tiganya Vincent-Mahakama -Dar es salaam
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Mustapher Siyani atakuwa Mgeni rasmi katika sherehe ya kuwaaga Majaji watatu kitaaluma wa Mahakama Kuu ambao wamestaafu.
Kwa mujibu wa taarifa,Majaji Wastaafu hao wataagwa Kitaalum katika Ukumbi Namba moja wa Mahakama Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam.
Majaji ambao wanatarajiwa kuagwa Kitaaluma ni pamoja na Mhe. Sekela Cyril Moshi, Mhe. Beatrice Rodah Mutungi na Mhe. John Samwel Mgetta, zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa Waraka Na. 1 wa Mwaka 2006 wa Jaji Mkuu.