Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mioango Bi. Jenifa Omolo akizungumza wakati akifungua semina ya kubainisha miradi itakayotekelezwa kwa ushirikiano baina ya sekta binafsi na serikali.
Kamisha wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) David Kafulila akifafanua mambo kadhaa Katika semina hiyo iliyoshirikisha Wadau mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Mioango.
……………………………..
SERIKALI imesema inafanyia kazi marekebisho ya sheria ili kujenga mazingira wezeshi kuvutia mitaji ya uwekezaji wa ubia kwenye sekta za nishati na uchukuzi kutoka sekta binafsi.
Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu Jenifa Omolo wakati akifungua semina ya kubainisha miradi itakayotekelezwa kwa ushirikiano baina ya sekta binafsi na umma.
Alisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa namna bora ya kupanga na kutekeleza miradi ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi.
Alitaja washiriki kwenye mafunzo wanatoka Shirika la Reli (TRC), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TIA), na kwamba kwa upande wa nishati Shirika la Umeme (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Mamlaka ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Alisema kuwa serikali imeandaa mafunzo haya kwa kushirikiana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) imewakutanisha pamoja wataalamu wa kimataifa ambao wanahusika na utaalamu wa uandaaji wa miradi, na mamlaka saba zikiwemo nne zinazohusika na sekta ya uchukuzi kwa lengo la kuwaongezea uelewa katika uandaaji na usimamiaji wa miradi nchini.
“serikali tuko tayari kuhakikisha tunavutia mitaji kutoka sekta binafsi kwa kufanya marekebisho kwenye seria na kanuni,”Omoli alisema.
Kwa upande wake Kamisha wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) David Kafulila, alieleza kuwa mitaji kutoka sekta bianfsi utaipunguzia mzigo serikali na hivyo kuwekeza kwenye amabzo hazina mvuto.
Alisema uwekezaji kwenye sekta za nishati na uchukuzi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu kwani utaharakisha maendeleo.
Kafulira alisema mpango wa serikali ni kuhakikisha sekta binafsi inachangia mtaji wad ola za kimarekani billion 9 sawa na trilioni 21 katika kipindi cha miaka mitatu.
“Rais Samia Suluhu Hassan ni kinara katika kusukuma ajenda ya sekta binafsi kuhakikisha kwamba inatoa mchango kwenye kuendesha uchumi, kwani inafahamika wazi kuwa ndio injini ya uchumi, na kwenye utekelezaji wa miradi ya ubia, sekta binafsi itekeleze baadhi ya maeneo ambayo serikali ingeyatekeleza,”.
Kwa mujibu wa Kafulira, serikali imeshafanya upembuzi yakinifu kwa baadhi ya miradi na kilichobaki ni kwa sekta binafsi kuwekeza kwenye utekelezaji wake akitoa mfano wa mradi wa barabara ya Kibaha- Chalinze, Mkoani Pwani.