Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni ametoa onyo kwa viongozi wa idara ya Maji Kata ya Kihurio wanaowatolea maneno machafu wananchi kuhusu kufaham bei mpya ya bili ya Maji ambayo imepagwa na Serikali
Dc Kasilda ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kata hiyo pia amemtaka Meneja wa maji (RUWASA)Wilaya Ya Same Abdallah Ally kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kupandishwa kwa bili ya Maji na kuendelea kutatua kero ya maji kwa wananchi ambao wanapata changamoto ya Maji
Aliendelea kumsisitizia Meneja wa Maji kufatilia kwa makini ili kuondoa kero hiyo kwa wananchi na waendelee kupata maji kwa wakati hasa kwenye kipindi hiki cha mvua na kuhakikisha vyazo vyote vya maji vilibomolewa na Mvua kukamilishwa katika Kata hiyo ya Kihurio na vijiji vingine.
Aidha DC Kasilda amewataka Wananchi kushirikiana kwa pamoja Serikali katika kuleta Maendeleo wilaya ya Same na kumuunga mkono Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukuza Uchumi.