MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa tuzo ya mshindi wa
kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kuwa na Sera Bora za Usalama na
Afya Mahali pa Kazi. (OSH)
Tuzo
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala
ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako kwenye kilele
cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi iliyokwenda sanjari na Maonesho ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi za umma na binafsi kwenye
viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro Ijumaa Aprili 28, 2023 na kupokelewa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki aliyefuatana na Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi, PSSSF Bw.Ernest Kihisombi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu CPA. Hosea Kashimba.
Kilele
cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi
hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine
duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha
uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi
ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni
kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”.
“Katika
mfuko suala la mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi na wanachama
wetu ni kipaumbele chetu, ukiangalia hata hapa kwenye banda letu, utaona hata
viti wanavyotumia watumishi wetu ni vile vinavyotakiwa kwa mujibu wa OSH.”
Alisema Bi. Zaida Mahavu, Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki
Akieleza
zaidi Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi alisema katika kuhakikisha
suala hilo linazingatiwa kikamilifu ofisi zote za PSSSF kote nchini zina
masanduku ya huduma ya kwanza (first aid kit) na wheel chairs.
“Lakini
pia wanachama nao hatukuwaacha nyuma, kwa wale ambao kutokana na hali yaafya au
umri huwa tunawafuata majumbani kwao wakati wa kipiti cha uhakiki wa wanachama.”
Alifafanua.
Akihutubia
katika kilelecha hafla hiyo, mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu –
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema
Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea
kusimamia masuala ya usalama na afya mahala pa kazi kwa kuwa ni haki ya msingi
ya kila mfanyakazi nchini.
Alisema
Mhe. Rais Samia amekuwa kinara katika kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa inalindwa
kwa kuendelea kuimarisha Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA).
Waziri
Ndalichako amewataka OSHA kuendelea kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi
kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na kuwahamasisha waajiri kuweka mifumo sahihi ya
usalama na afya katika maeneo yao ya kazi na kuendelea kuzingatia sheria na
kanuni za usalama na afya sehemu za kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akimkabidhi tuzo Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki Bi. Zaida Mahavu aliyefuatana na Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi, PSSSF Bw. Ernest Khisombi
Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi, PSSSF Bw. Ernest Khisombi, akimuhudumia mwanachama aliyetembelea banda la PSSSF. Aliyesimama ni Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini, Bi. Zaida Mahavu.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini, Bi. Zaida Mahavu akimkabidhi kipeperushi chenye taarifa za PSSSF, mwanachama wa Mfuko, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma.
Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi, PSSSF Bw. Ernest Khisombi, aki (watatu kushoto) na Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki , Bi. Zaida Mahavu (watatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya PSSSF inayoshiriki maonesho hayo.