Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wanaofanya kazi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dodoma leo Aprili 29, 2023 wamefanya matembezi mafupi yenye lengo la kuimarisha afya kwa askari hao. Matembezi hayo yameongozwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Idrisa Burah, huku akiwataka askari hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiuepusha na
maradhi nyemelezi ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye hafanyi mazoezi.