Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamewakamata watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo katika kijiji cha Nanjilinji, Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi.
Akizungumza baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Kamishna Msaidizi anayesimamia shughuli za uhifadhi katika Kanda ya Kusini Mashariki, Kennedy Sanga amesema TAWA imeimarisha kitengo cha intelijensia kinachofuatilia kwa kina taarifa zote za ujangili ndani na nje ya maeneo ya hifadhi.
Kadhalika, Kamishna Sanga amesema, ujangili wa wanyamapori unaharibu mfumo ikolojia wa uhifadhi na amewataka wakazi wa maeneo hayo kuacha mara moja, kwani ni makosa ya kiuhujumi uchumi.
“majangili wote wenye nia ya kuua tembo waache vitendo hivyo kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo” ameongeza Kamishna Sanga.