Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, iliyoratibu maandalizi ya filamu ya Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi, amesema
mwaka mmoja leo, tangu filamu hiyo izinduliwe hapa nchini, takribani watu bilioni 1.2 duniani, wameiona au kujihusisha na filamu hiyo kupitia kupata taarifa za vyombo mbalimbali vya habari.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Aprili 28, 2023 alipokutana na wanahabari jijini Dodoma ikiwa ni mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoizindua filamu hiyo jijini Arusha mwaka jana.
“Mwaka mmoja leo Royal Tour imeleta mafanikio makubwa sana ikiwemo kuongeza watalii nchini maradufu, mapato ya utalii kuongezeka maradufu na hata mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuongeza miruko ya kuja nchini,” alisema Dkt. Hassan Abbasi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.