Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi na wazazi wakati wa mahafali ya
kidato cha sita ya Shule ya Wasichana ya Iringa leo Aprili 27, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akiangalia picha iliyochorwa na wanafunzi alipotembelea
maonesho alipowasili katika Shule ya Wasichana ya Iringa alipowasili kwa ajili
ya kushiriki mahafali ya kidato cha sita alipofanya ziara mkoani Iringa leo Aprili
27, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akipata maelezo kuhusu mafunzo ya sayansi kwa vitendo
kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Iringa alipowasili kwa ajili ya
kushiriki mahafali ya kidato cha sita alipofanya ziara mkoani Iringa leo Aprili
27, 2023.
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Iringa wakiwa katika
mahafali ya kidato cha sita leo Aprili 27, 2023 ambapo mgeni rasmi alikuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akimtunuku cheti cha kuhitimu kidato cha sita mmoja wa
wahitimu katika Shule ya Wasichana ya Iringa alipowasili kwa ajili ya kuongoza
mahafali ya kidato cha sita aliposhiriki mahafali hayo mkoani Iringa leo Aprili
27, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha sitammoja wa wahitimu katika Shule ya Wasichana ya Iringa wakati wa mahafali ya kidato cha sita mkoani Iringa leo Aprili 27, 2023.
……………………………….
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo amesisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa shule na
taasisi ili kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Amesema hayo leo Aprili 27, 2023 wakati akizungumza na wanafunzi, walimu
na wazazi wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha sita katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana ya Iringa.
Dkt. Jafo amesisitiza katazo la matumizi ya kuni na mkaa lililotolewa na
Serikali hivi karibuni haliwahusu watumiaji wadogo bali kwa taasisi zinazolisha
watu kuanzia 100 na kuendelea.
Amesema ekari za miti zinapotea kwa kukatwa na ndio maana Serikali
inasimamia kampeni mbalimbali za upandaji wa miti kote nchini ikiwemo
‘Kampeni ya Soma na Mti’ ili kukabiliana na changamoto za kimazingira.
Amesema katika kuunga mkono hatua hiyo Kampuni ya Gesi ya Taifa
inatarajia kufunga mtungi wa nishati hiyo katika Shule ya Wasichana ya Iringa
hatua itakayosaidia kusitisha matumizi ya kuni.
“Tuna dhamana ya utunzaji mazingira kwa kuacha kukata miti ,ndio maana
nilitoa maelekezo kuhusu matumizi ya nishati safi kwani matumizi ya gesi
huokoa fedha ambazo zinatumika kwa ajili ya kuni na mkaa kwa ambazo ni
shilingi milioni tano hadi nane kwa mwezi.
“Ukiangalia katika matumizi ya gesi kwa mwezi tani moja ni shilingi milioni
mbili kule katika Shule ys Sekondari Ruvu nilikuwepo juzi wameanza kutumia
gesi na kuachana na matumizi ya kuni sasa lengo letu itafikia muda tutaacha
kabisa kutumia kuni,” amesisitiza.
Dkt. Jafo ameipongeza Jumuiya ya shule hiyo kwa upandaji wa miti kusema
kuwa iwe ya mfano kwa shule zingine nchi ili kusukuma mbele ajenda ya
utunzaji wa mazingira inayosisitizwa na viongozi wa Serikali.
Pia, amewataka wahitimu hao na wanafunzi kwa ujumla kutojihusisha na
vitendo vinavyoenda kinyume cha maadili kwani vitawaharibia maisha yao
hivyo kuharibu ndoto zao.