…………….
Na Victor Masangu,Kibaha
Mlezi wa umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mji Selina Koka katika kuisaidia jamii amesema ataendelea kushirikia na wanawake wajane kwa kuwawezesha mitaji mbali mbali ambayo itaweza kuwasaidia kuondokana na wimbi la umasikini.
Selina ameyaesema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti aa UWT Wilaya ya Kibaha mji katika kata ya Viziwaziwa ambapo ameambatana na wajumbe wa kamati ya utekelezaji pamoja na baadhi ya madiwani wa viti maalumu.
Mama Koka alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mipango madhubuti ambayo itaweza kuwasaidia wajane ambao ni wajasiriamali kuendesha shuguli zao mbali mbali za kujipatia kipato ili waweze kujikimu kimaisha.
“Natambua katika kata hii ya Viziwaziwa Kuna makundi ya wanawake ambao ni wajane hivyo kwa Upande wangu nitaendelea kutoa sapoti na kuwashika mkono kwa hali na mali ndio maana naendelea kuwapa mitaji,”alisema Selina.
Kadhalika mama Koka ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi laki tano kwa wanawake wa uwt kata ya Viziwaziwa na kwamba ametoa fedha kwa ajili ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuhifadhia fedha hizo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja alimpongeza Mama Koka kwa kuwakumbuka wanawake katika kuwawezesha kiuchumi katika nyanja mbali mbali.
MWISHO