Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Bw. Silvery Maganza akizungmza na waandishi wa habari Kando ya mkutano wa uwasilishaji wa ttafiti zilizofanywa na ili kuboresha huduma hiyo ya Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Alhamisi Aprili 27,2023.
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) umefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 31 kutoka katika michango ya wanachama milioni 4.4 katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2023.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Aprili 27 ,2023 katika Mkutano wa kuwasilisha tafiti
Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) Mratibu wa Mfuko huo kutoka Ofisi ya Ras Tamisemi, Bw. Silvery Maganza, amesema kuwa kutokana na michango ya wanachama ni zaidi ya bilioni 23 zimerejeshwa kwa watoa huduma ikiwemo malipo ya gharama zilizotumika kuwahudumia wanachama.
Bw. Maganza amesema kuwa tafiti zimebainisha kuwa jamii inauhitaji mkubwa wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) hasa katika utoaji wa huduma ya afya.
Amesema kuwa asilimia 92 taasisi mbalimbali kutoka sekta zisizo rasmi wameonesha nia ya kushirikiana na mfuko wa CHF katika kutangaza ili kufikisha taarifa sahihi iliyokusudiwa.
“Taarifa hizi zinakwenda kuboresha mfuko wa CHF ili iweze kutoa huduma bora kwa jamii kama ambavyo imekusudiwa” amesema Bw. Maganza.
Amesema kuwa taarifa za utafiti zinakwenda kuleta mafanikio makubwa katika kuboresha huduma ya mfuko wa CHF katika jamii kwani wadau mbalimbali wameonesha nia ya kujiunga na mfuko huo.
CHF ni Mfuko wa Bima wa afya ya Jamii iliyoanzishwa na serikali Kwa lengo la kuhudumia wananchi ambao wapo katika sekta ambazo sio rasmi ikiwemo wakulima, wafugaji, wafanyabiashara ndogo ndogo pamoja na jamii ambayo ipo katika sekta isiyo rasmi.
Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ulifanya utafiti wake ambao matokeo yake yanatarajiwa kuchangia katika utungaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa Wote (UHI).
Wawasilishaji mbalimbali wakijadiliana mara baada ya uwasilishaji wa utafiti huo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali zikiwaonesha washiriki wa mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam wakifuatilia majadiliano kuhusu uboreshaji wa Mfuko wa Afyaya Jamii CHF.