Wizara ya Madini imetoa vipaumbele vyake kwenye mwaka wa fedha 2023/2024 kwenye lengo la kuhakikisha sekta ya madini inachangia kujenga uchumi imara na kuongeza pato la Taifa kupitia rasilimali Madini.
Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema Wizara ya madini imepanga kutekeleza vipaumbele 6 ambavyo ni.
1. Kuimarisha Ukusanyaji wa Maduhuli na Kuongeza Mchango
wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa.
2. Kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati.
3. Kuwaendeleza na Kusogeza Huduma za Ugani kwa
Wachimbaji Wadogo.
4. Kuhamasisha Shughuli za Uongezaji Thamani Madini.
5. Kuhamasisha Uwekezaji na Biashara katika Sekta ya Madini
6. Uanzishwaii wa Minada na Maonesho ya Madini ya Vito
7. Kuzijengea Uwezo Taasisi zilizo Chini ya Wizara ya Madini ili
Ziweze kutekeleza Majukumu Yao kwa Ufanisi Zaidi
Waziri Biteko ameyasema hayo wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya Wizara ya Madini Bungeni, Dodoma.