Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe akifungua mkutanomkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam Aprili 27,2023.
……………………………………………
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi nchini wametakiwa kuwa na utamaduni wa kujiandaa mapema kustaafu kwa kutengeneza mazingira rafiki ya kiuchumi jambo ambalo litawasaidia kuishi maisha ya heshimu katika jamii kipindi wanapostaafu.
Akizungumza leo tarehe 27/4/2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Mwaka, Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe, amesema mkutano mkuu huo umelenga kufanya uchaguzi wa viongozi, kujadili mpango mkakati, Bajeti pamoja na kupitisha mpango kazi wa mwaka 2023.
“Tunatarajia katika mkutano huu kuchangua viongozi watakaotuongoza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo” amesema Bi. Rubambe.
Bi. Rubambe amesema kuwa lengo la Chama hicho ni kujitoa katika kusaidia na kufanya kazi za jamii pamoja na kuendeleza umoja na mshikamano na mahusiano kwa wastaafu hao ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwa wastaafu kwa vijana ambao wako kazini na wanaoingia kazini kwakuwa ni wastaafu watarajiwa.
“Wakati umefika kwa wafanyakazi kujipanga na kujiandaa mapema kustaafu ili kuleta tija katika maisha” amesema Bi. Rubambe.
Miongoni mwa washiriki katika mkutano mkuu wa mwaka alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba ambapo ameshiriki kama mwanachama wa heshima.
Naibu Gavana mastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Bernald Kibese ambaye pia ni Mwanachama wa heshima ameshukuru chama cha BOTRA kwa kuwaalika wanachama wa heshima wa BOTRA katika mkutano mkuu huo ambapo pia amewatakia mkutano mwema ili malengo ya mkutano yakatimie.
Naye Afisa Usajili Kanda ya Mashariki Bi. Salama Semakalila ambaye amemuwakilisha Bw. Emmanuel Kihampa Msajili wa Jumuiya za Kiraia amewataka wastaafu hao kuhakikisha wanafanya uchaguzi na kupata viongozi ikiwa ni pamoja na kuepusha migogoro isiyoya ya lazima pamoja na kuhakikisha wanapeleka katika ofisi ya msajili taarifa zote za mkutano huo mkuu ili uweze kupata baraka msajili.
Naibu Gavana mastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Bernald Kibese akitoa salamu zake kwa niaba ya wanachama wa heshima wa chama cha wafanyakazi wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania BOTRA kwenye mkutano uliofayika kwenye ukumbi wa BoT jijini Dr Esa Salaam.
Afisa Usajili wa Jumuiya za Kiraia Kanda ya Mashariki Bi. Salama Semakalila akizungumza katika Mkutano Mkutano Mkuu wa BOTRA uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe pamoja na viongozi wengine wakisimama kwa ajili ya kuwakumbuka wananchama wastaafu waliotangulia mbele ya haki.
Picha mbalimbali zikionesha wastaafu wakishiriki katika mkutano mkuu huo wa mwaka.