Wananchi wa kijiji cha Izindabu kata ya Rugata Wilaya ya Sengerema Halmashauri ya Buchosa Mkoa Mwanza Wameishukuru mamlaka ya wanyamapori Tanzania kwa kusikia kilio chao na kufika kuwaua mamba waliokuwa wakiwavamia wanakijiji hao.
Mamba hao walikuwa wakidhuru hadi kuwaua wananchi waliokuwa wakipita na kuchota maji kwenye ziwa na kupelekea wanakijiji wa eneo hilo kuishi kwa mashaka na kukosa amani.
“Katika maeneo haya kijiji hiki cha Izindabu kimekuwa kikitajwa sana kuwa na matukio mengi ya kushambuliwa na wanyama wakali wakiwemo Mamba, na nyakati zote tumekuwa tukiripoti TAWA kutokea kwa matukio haya. Tunaishukuru sana TAWA wamekuwa wakija na leo wamefanikisha kutusaidia.”- Diwani kata ya Rugata
Mpaka sasa TAWA imeua mamba wawili na zoezi la kuweka ulinzi na usalama kwa wananchi wa kijiji hicho bado linaendelea.