Na WAF, BUNGENI DODOMA
NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema katika mwaka wa fedha 2022-2023 Serikali kupitia Wizara ya Afya imejenga nyumba za Watumishi 52 zenye thamani ya Shlingi Bilioni bilioni 3,417,556,981 katika hospitali za Rufaa za Mikoa na Hospital za kanda ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Dkt. Mollel amesema hayo leo Aprili 25 Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Dkt. Ritta Enespher Kabati katika Mkutano wa kumi na moja.
Amesema, “katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imejenga nyumba 52 za watumishi zenye thamani ya shilingi bilioni 3,417,556,981 katika Hospitali za Kanda na Hospitali za Rufaa za Mikoa ikiwemo nyumba 1 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.”
Ameendelea kusema kuwa, Serikali itaendelea kujenga nyumba kwaajili ya Watumishi ili kuwapunguzia hadha, jambo linaloongeza hamasa katika utendaji wao na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Aidha, Dkt Mollel amesema, Serikali itaendelea kuboresha utoaji huduma kwa wananchi, ikiwemo kuajiri Wataalamu wa afya, huku akisisitiza zoezi la kuamisha Wataalamu hasa madaktari bingwa kulingana na mzigo wa wagonjwa wa kituo husika na kuendelea kuwaendeleza watumishi kupitia mafunzo ya ndani na nje ya nchi ni mkakati mwingine wa kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.