Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Bernard Konga akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati Mfuko huo ulipokutana nao kwenye ukumbi wa Ofisi za Takwimu NBS jijini Dodoma.
Wahariri mbalimbali wakipata maelezo wakati walipotembelea Katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Wahariri Kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mada Katika kikao kazi kati Yao na NHIF kilichofanyika kwenye ukumbi wa NBS jijini Dodoma.
………………………..
Na Angela Seth – Dodoma
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF umewekeza shilingi Bilion mia moja ishirini na tisa katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Mkoani Dodoma ambapo fedha hizo zimewekezwa kwenye majengo ya hospitali hiyo pamoja na vifaa tiba ziwemo mashine za X ray , CT-Scan yenye thamani ya shilingi Bilion 1.6 iliyoanza kutumika 2017.
Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo walipotembelea hospitali katika ya Benjamin Mkapa kujionea namna NHIF walivyowekeza Dkt. Furaha Malecela amesema anawashukuru NHIF kwa uwekezaji waliofanya kwenye hospitali hiyo kwani imekuwa kimbilio kubwa na sasa wameweza kuhudumia wagonjwa kutoka sehemu mbali nchini
Dkt.Malecela ameongeza kuwa pia kumewekwa mfumo wa kuchuja damu katika hospitali ya hiyo ambao umewezeshwa na NHIF huu ni msaada Kwa watu wengi wenye matatizo ya Figo ambao wanaokuja kufanyiwa huduma hiyo mara tatu kwa wiki ambapo Hadi sasa wagonjwa 65 wanapewa huduma ya kuchujwa kwa damu kwenye hospitali hiyo.
Aidha Kwa upande wake Mwenyekiti WA Jukwaa na wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile amewashauri NHIF kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi ili weweze kupata uelewa zaidi kuhusu bima ya Afya kwani kuna baadhi ya wananchi bado hawajapata elimu ya kutosha vile vile kutumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kurusha matangazo mbali mbali yanayohamashisha wananchi kujiunga na Bima hiyo na kueleza faida zake kiundani zaidi.
Balile pia ameshauri NHIF kuwaalika wanasiasa na kuwapeleka kwenye maeneo mbalimbali waliyowekeza ikiwemo hospitali ya Benjamin mkapa pamoja na kuweka wazi Mawasiliano ili wananchi waweze kuwasiliana nao moja kwa moja kueleza kero wanazokumbana nazo katika matumizi ya bima za Afya.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko WA Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw. Bernard Konga amesema mfuko huo ulioanzishwa Mwaka 2001 ambapo lengo kuu ilikuwa kupatikana kwa huduma za Afya kwa wananchi mbalimbali amesema mfuko huo utaendelea kutoa elimu na amewaomba wananchi kujitokeza kujiunga na Bima ya Afya mara wanapotata ujumbe kupitia elimu wanayoitoa kwa kufanya hamasa kupitia mabonza, nyumba za Ibada magulio, vikao vya wazazi na mikutano ya hadhara hata hivyo amewaomba wanachama kukata bima wakiwa bado wazima kwamba wasisubiri hadi waugue ndio wakate bima kwakuwa moja ya changamoto zinazoukumba mfuko huo ni kuonekana wanachama wengi hujitokeza kuchukua kadi za Afya wakiwa tayari wanaumwa.
Hata hivyo mfuko huo una mpango wa kuunganisha mfumo wake wa kieletroniki na mfuko mingine au Taasisi mbali mbali za serikali ikiwemo NIDA, RITA, NSSF, BRELA , WCF na TRA ili kurahisisha utambuzi, Uhakiki, na Usajili wa wanachama na kampuni binafsi.
Kuhusu Toto Afya Card kushidwa kujiendeleza Mkurugenzi amesema mzigo huo ulikuwa mkubwa kwani watoto wengi waliingizwa kwenye Bima hiyo wakiwa tayari wanaumwa ambapo kwa kipindi cha muda mfupi Toto Afya Card ilikusanya bilion 5 na kutumia Bilion 40 na kupelekea mfuko huo kupata hasara ya Bilion 35.