Kamishna wa Ubia kati ya Sekta Binafsi na Serikali (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. David Kafuli akizungumza Katika kikao kazi kati ya Wizara hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari wanaofanya kazi Kwa karibu na Wizara ya Fedha kilichofanyika Hazina Ndogo ya Wizara ya Fedha Jijini Arusha.
…………………………………………..
NA JOHN BUKUKU, ARUSHA.
Wawekezaji nchini wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kufanya Uwekezaji wa ujenzi wa miundombinu kupitia mfumo wa ubia kati ya Sekta Binafsi na Serikali (PPP) kutokana kuwa na uhitaji mkubwa kadri wakati unavyozidi kwenda mbele.
Imeelezwa kuwa uwekezaji wa ujenzi wa miundombinu kupitia mfumo wa ubia kati ya Sekta Binafsi na Serikali (PPP) watumiaji wa miundombinu watakuwa wanachangia gharama ili kuleta tija katika kufanikisha miradi kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumza leo Jumanne Aprili 25, 2023 Katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari wanaofanya kazi Kwa karibu na Wizara ya Fedha kinachofanyika Hazina Ndogo ya Wizara ya Fedha Jijini Arusha, Kamishna wa Ubia kati ya Sekta Binafsi na Serikali (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. David Kafulila, amesema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa Profesa Benno Ndulu unaonesha mahitaji ya miundombinu bado ni mkubwa katika kufanikisha mipango ya maendeleo.
Bw. Kafulila amesema kuwa miundombinu iliyopo ni sawa na 1/3 ya miundombinu hadi kufikia mwaka 2050.
Amesema hatuwezi kujenga miundombinu yote kwa fedha ya kodi, hivyo ushirikiano na sekta binafsi unaitajika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kufikia malengo tarajiwa katika kuhakikisha tunapiga hatua.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongoza na Rais Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassan imefanya mambo mengi makubwa ikiwemo kutengeneza sheria shindani ambazo zitakuwa na tija katika kuhakikisha tunafikia malengo kwa kufanya uwekezaji kupitia sekta binafsi” amesema Bw. Kafulila.
Amesema kuwa serikali inatarajia kuwajengea uwezo wataalamu jambo ambalo litasaidia kunufaika na mikataba ya wabia katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, afya, elimu pamoja na reli.
Ameeleza kuwa kuna miradi mikubwa ambayo ujenzi wake unaendelea ikiwemo mradi wa BRT, huku akibainisha kuwa serikali inatarajia kujenga Hoteli ya nyota tano katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Majengo ya kibiashara pamoja na ujenzi wa barabara kutoka Kibaha hadi Chalize wenye urefu wa kilometa 78.9 , Chalize ambapo itaendelea hadi Morogoro.
“Ujenzi wa barabara ya Kibaha hadi Chalize tayari utaratibu wake umekamilika sasa anatafuta mwekezaji, lakini pia tunatarajia kujenga barabara ya mwendo kasi ya kulipia ambayo haitakuwa na askari wa barabarani, katika eneo hilo ambalo ambalo lina msongamano mkubwa wa magari tuna imani itakapojengwa barabara hiyo itasaidia sana kupungumza msongamano hivyo kuchochea zaidi shughuli za maendeleo” amesema Bw. Kafulila.
Bw. Kafulila ameeleza kuwa asilimia kubwa ya magali yanayobeba mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam yanapita katika barabara ya Morogoro, hivyo tunatarajia kufanya uwekezaji huo ili kuleta tija kwa maendeleo ya Taifa.
Amesema lengo ya serikali ni kutekeleza miradi mingi na mikubwa kwa kutumia mfumo wa ubia kati ya sekta binafsi na serikali ambao utakuwa na tija katika uwekezaji wake.
“Mikopo na kodi haiweze kujenga miradi ya miundombinu mbalimbali, tunapaswa kushirikiana na sekta binafsi ili kujenga maisha bora na uhakika kwa watanzania” amesema Bw. Kafulila.
Amebainisha kuwa lengo la serikali katika mpango wake wa miaka mitano ijayo imeweka wazi inatarajia kutumia trillion 114, huku trillion 21 zikitokana na mfumo wa PPP.
Katika hatua nyingine amebainisha kuwa mwezi Mei mwaka huu wanatarajia kufanya warsha na taasisi mbalimbali za umma kwa ajili ya kueleza mipango na matarajio yao pamoja kuwakutanisha na wataalamu kutoka nje ya nchi ili kujengewa uwezo wa namna ya kutekeleza miradi kupitia PPP.
“Wananchi wanatakiwa kuwa na utayari wa kutoa ushirikiano wa utekelezaji wa miradi kupitia PPP ili kuondoa changamoto za kukopa kwa ajili ya Ujenzi wa miradi” amesema.
Amefafanua kuwa kadri muda unavyozidi kwenda hatuwezi kutekeleza miradi kupitia mikopo hivyo wananchi wanapaswa kuwa na utayari wa kulipia gharama za miundombinu ambayo inatarajia kujengwa.
Kamishna wa Ubia kati ya Sekta Binafsi na Serikali (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. David Kafuli akisisitiza jambo wakati akizungumza Katika kikao kazi kati ya Wizara hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari wanaofanya kazi Kwa karibu na Wizara ya Fedha kilichofanyika Hazina Ndogo ya Wizara ya Fedha Jijini Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wiara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja kulia akiwa ameketi pamoja na Mwenyekiti wa wahariri katika kikao kazzi hicho Bw. Benny Mwang’onda kutoka Azam Media wakifuatilia mada katika kikao kazi hicho.
PIcha zikioneshambaadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia uwasilishaji uliokuwa ukifanyika katika kikao kazi hicho.
Kamishna Msaidizi wa Sera za Uchambui wa Uchumi Wizara ya Fedha Bw. Mbayani Yudica Saruni akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya serikali katika kikao kazi hicho.
Kamishna Msaidizi wa Sera za Uchambui wa Uchumi Wizara ya Fedha Bw. Mbayani Yudica Saruni akisisitia jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya serikali katika kikao kazi hicho.