Na Stamil Mohamed
Wananchi wametakiwa kushiriki shindano la uandishi wa mtandao wenye kuteja tija msimu wa tatu katika nyanja utawala Bora na uwajibikaji kuleta mabadiliko chanya na maendeleo kwenye jamii.
Akizingumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Forums Bw. Maxence Melo amesema shindano hilo linatarajiwa kufanyika Kwa siku 90 ambapo litaanza tarehe 1 Mei na kuwataka wananchi kuandika maudhui mbalimbali yanayolenga kuchochea mabadiliko chanya na kupeleka kuwepo Kwa uwajibikaji na Utawala Bora.
Aidha amesema mgeni rasmi katika kilele Cha mashindano hayo anatarajiwa kuwa Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete huku jopo la majaji wa mashindano hayo likiwa ni Wataalamu wa Tano wa mambo ya utawala bora na uwajibikaji ambao ndiyo wataamua kupatikana Kwa washindi kulingana na vigezo vilivyowekwa huku kura za majaji zikibeba 60%ya ushindi, na kura za wananchi jukwaani zikibeba 40% ya ushindi ambapo washindi watato wa shindano Hilo watapata zawadi ya Mil. 20.
Hata hivyo kufanyika Kwa shindano la msimu huu ni baada yakufanikiwa Kwa shindano la mwaka 2021 na 2022 Kwan miongoni mwa maudhui yaliyowasilishwa yamechangia maboresho katoka mifumo ya utoaji huduma serikalini huku baadhi ya taasisi zikipokea mapendekezo kuahidi kuyafanyia kazi.