GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amewahimiza Watanzania kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji
na hivyo kukuza uchumi.
Bw. Tutuba ameyasema hayo katika hafla
ya futari aliyowaandalia viongozi wa Serikali, Jumuiya ya wenye Mabenki, Watoto
wa Madrasa na Makundi Maalum kwenye Makao Makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam
Aprili 20, 2023.</
“Sisi kama Benki Kuu tunaendelea kusimamia
uchumi wa nchi yetu na niwahakikishie uchumi wetu uko imara, mfumuko
wa bei umedhibitiwa na fedha yetu pia iko imara, sekta ya fedha inazidi kukua.”
Alisema Bw. Tutuba na kuongeza .. “Ninachoomba kutoka kwenu ni ushirikiano, tufanye
kazi kwa bidii ili tuzalishe zaidi kwani hiyo ni nyenzo muhimu katika kujenga uchumi
imara.” Alifafanua.
Gavana huyo wa BoT alisema Benki Kuu
ya Tanzania kwa umakini mkubwa itaendelea kusimamia ustahimilivu wa uchumi, sera ya fedha, mfumuko wa bei,utoaji
wa leseni kwenye taasisi za fedha, udhibiti sekta ya fedha na usimamizi wa mauzo
ya nje.
“Juzi nilikuwa kwenye Mikutano ya Benki ya Dunia (WB) wameisifu nchi yetu kwa usimamizi mzuri wa uchumi ikilinganishwa na
Mataifa mengine.” Alidokeza.
Aidha Gavana Tutuba aliwashukuru wote walioitikia mwaliko wa
BoT kuja kujumuika na watumishi wa Benki hiyo katika sadaka hiyo ya futari.
Tukio kama hili tunalifanya kwenye matawi yetu yote Saba (7)
na lengo kwakweli ni kuungana na jamii katika kufanya matendo mema yanayompendeza
Mungu.
“Kufunga, kusali kutoa sadaka ni mambo ambayo Mwenyezimungu huyapokea
kwa haraka.” Alisema Bw. Tutuba.
Awali akitoa Mawaidha kuhusu “Uislamu
na Uchumi” kabla ya futari, Imam wa Msikiti wa Maamour Upanga jijini Dar es Salaam,
Sheikh Issa Othman (Mufti London), alisema ipo misingi sita (6) inayoelezea Uislamu
na Uchumi ambayo ni udugu, Naswiha, kuheshumu makubaliano, Hofu ya Mungu, na huruma.
Sheikh Othman pia alisema, Nidhamu
ni jambo muhimu sana katika Uislamu.
Funga ya Mwezi Mtukufu
wa Radhan, inajenga nidhamu binafsi mambo ambayo yanahimizwa katika uislamu.
Akifafanua alisema, Nidhamu hiyo imegawanyika
katika sehemu tatu ambazo ni active diceplin, reactive dicepli (inafundisha ustahikilivu
kwamba hata unapochokozwa hupaswi kujibiza na mwisho ni proactive deciplin (mambo
ambayo umeyazingatia au kuyafuata wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
uendelee kuyafuata hata baada ya kumalizika kwa Mfungo.
Naye Sheikh Muharram Mziwanda aliwahimiza
Watanzania kwa ujumla kuendelea kuenzi Amani na Utulivu nchini kwani mafanikio ya
kukua kwa uchumi yanategemea sana hali ya Amani na Utulivu wa nchi.
“Uchumi hauwezi kusogea ikiwa Msingi wa uchumi
haupo (utulivu), tuhakikishe tunaendelea kuenzi Amani na Utulivu kila mmoja kwenye
nafasi zetu,” alisema Sheikh Mziwanda.
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.
Imam wa Msikiti wa Maamour Upanga jijini Dar es Salaam, Sheikh Issa Othman (Mufti London),
Wageni waalikwa
Wageni waalikwa
(Picha zote na BoT).