Viongozi wa Dini wameaswa kuendelea kutoa Elimu kwenye Nyumba za ibada kukemea Ukatili wa kijinsia na maadili yasiyo kubalika ikiwemo Mapenzi ya Jinsia Moja, kulinda Mila na Desturi pia heshima ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Babu amebainisha hayo katika Hafla ya Iftaar alipo wakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiry Mkalipa iliyo andaliwa na mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni Nyumbani kwake kwa ajili ya Viongozi mbalimbali wa madhehebu ya Dini,vyama vya Siasa na makundi mbalimbali wakiwemo waendesha pikipiki.
Mkuu huyo wa Mkoa Mgeni rasmi aliyewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Hai amesema kutokana na wimbi la Mmomonyoko wa maadili unaosababishwa na baadhi ya watu wasio na nia njema kueneza Michezo isiyo kubalika ikiwemo kuhamasisha mapenzi ya Jinsia Moja, viongozi wa Dini wananafasi kubwa ya kuongea na Jamii kuwatahadharisha juu ya madhara ya Tabia hiyo ambavyo pia haimpendezi mwenyezi mungu.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewashukuru viongozi wa madhehebu ya Dini na watu wote walio shiriki Hafla hiyo kupata Iftaar, nakuwasihi kuendeleza mshikamano katika kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
“Kwa dhati ya Moyo wangu niwashukuru Sana Viongozi wa Dini, vyama vya Siasa na wote mlio jitokeza kwa kujumuika Katika Hafla hii ya Iftaar, hakika nimefarijika kuona idadi kubwa ya watu mlio jitokeza, niombe ushirikiano huu uendelee pia kwenye masuala mengine tuweze kusongesha Gurudumu la maendeleo kama ilivyo dhamira ya Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Wakitoa salamu za shukrani baadhi ya viongozi akiwemo Shekhe mkuu wa Wilaya ya Same Idd Bin Juma, pamoja na Askofu mstaafu wa Jimbo katoliki Wilaya ya Same Jacob Koda, wamesema ushirikiano wanaopata toka kwa viongozi wa serikali ikiwemo kushirikishwa katika mambo mbalimbali itasaidia kuleta umoja wa kufanikisha masuala mbalimbali ikiwemo hayo ya kukabiliana na matukio ya Ukatili na mipango ya maendeleo.