Na Mwaandishi wetu.
Kutokana na sakata la uuzwaji wa kampuni ya Tanga Cement kumekuwa na mijadala mingi
juu ya uuzwaji wa asilimia 68.33 ya hisa za Tanga Cement PLC ambapo mijadala hii imeibua
sintofahamu kwenye jamii kutokana na watu wengi kutoelewa juu ya mchakato mzima na
faida itakayo patikana endapo kampuni ya Scancem Internationa Da itafanikiwa kununua
hisa hizo.
Kutokana na wasiwasi pamoja na malalamiko kutoka kwa wazalishaji wengine wa simenti
nchini juu ya uuzwaji kwa kampuni ya Tanga Cement ambako kutasababisha mwekezaji
mmoja kutawala soko la simenti nchini na hii kumwezesha mzalishaji mmoja kumiliki asilimia
zaidi ya 35 la soko la simenti nchini, hii taarifa si kweli.
Mmoja ya wafanyakazi wa kampuni ya Tanga cement ambae hakutaka jinalake litajwe
ameeleza kuwa Endapo mtu atajaribu kufanya utafiti rahisi tu ambao hauhitaji gharama
kubwa na kuweza kujua idadi ya viwanda vya simenti nchini ambavyo vinazalisha kwa
ukamilifu na vile ambavyo husaga simenti, atakutana na idadi kubwa ya viwanda hivyo.
Viwanda hivi huzalisha zaidi ya kile ambacho nchi yetu inaweza kutumia. Kwa lugha
nyingine tunaweza sema kuwa usambazaji wa bidhaa ni zaidi ya uhitaji wa sokoni. Hivyo
hakuna namna ambavyo mzalishaji mmoja anaweza kutawala soko lililo na wazalishaji
wengi.
Tukiitazama kampuni ya Tanga Cement PLC, kwa takribani miaka 5, imekuwa ikipata hasara
kutokana na gharama za unedeshaji hasa kupitia taarifa ambazo tumekuwa tukizisoma
kwenye vyanzo mbalimbali, sababu zilizoelezwa kuwa ni kupanda kwa gharama za
uendeshaji ikiwepo nishati na usafirishaji.
Endapo ununuzi huu utafanikiwa, ni dhahiri kuwa kampuni ya Scancem Da, itatakiwa
kurekebisha hali ya kampuni hasa upande wa kiufundi, na kuhakikisha kiwanda
kinaendeshwa vizuri kwa faida ambayo watanzania wote watanufaika kutokana na
upatikanaji kwa bidhaa muda wote huku Serikali ikiendelea kujipatia mapato ambayo Tanga
Cement kwa kipindi kirefu ilishindwa kulipa kwa muda mrefu.
Tanga Cement itabadilika kutoka kampuni iliyokuwa inapata hasara na kuwa kampuni
inayotengeneza faida. Kwa ujumla, ununuzi huu utaleta mfumo mpya wa undeshaji wa
viwanda vya simenti nchini kutoka na na mabadiliko haya. Labda wazalishaji wengine wana
wasiwasi kutokana na changamoto ya kiteknolojia ambapo itawalazimu kubadilika
kiteknolojia ili kuweza kuendana na ushindani.
Uuzwaji wa Tanga Cement unaungwa mkono na wadau wote wakubwa na wadogo pamoja
na wafanyakazi wote wa Tanga Cement.
Mwandishi wetu alijaribu pia kumpigia simu moja na marafikizake wanaofanya kazi kwenye
kampuni hiyo ili kujua hisia zao juu ya suala hii maoni yake yalikuwa kama haya. “Yaani ni
kama wanatuchelewesha tu, tunaisubiri kwa hamu siku ambayo mpango huu utakamilika.
Wote tuna furaha kutokana na hali yetu ya sasa.
Hatuhitaji kufikia hali ya mpaka kukosa mshahara kama hali hii itaendelea kwa muda mrefu.
Tunaiona kampuni ya Scancem International Da kama mkombozi wetu na aliyekuja
kurudisha hali nzuri ya kampuni yetu.
Sambamba na hilo tunahitaji serikali sikivu itusaidie kwenye changamoto ambazo kama
kampuni tunapitia magumu sana.
Kwa mfano, kwa sasa kiwanda kinazalisha chini ya kiwango kutokana na changamoto ya
umeme, Hata pale tunapozalisha hiko kidogo, unakuta hakuna mabehewa ya kutosha ya
kusafirisha simenti kwenda sokoni”.
Alisema; “ Sijui kwanini watu wengine ambao sio wahusika wa moja kwa moja au waathiriwa
na biashara ya simenti au mchakato huu mzima wanaingilia suala hili. Aliendelea kusema
“Kwa mfano huyu Chalinze Cement ambaye sio hata mzalishaji au muuzaji.
Alieleza kuwa huyu jamaa ana duka la rangi jijini Dar es Salaam. Na sasa hata baadhi ya
wateja wanacheza mchezo huu kutokana na hawa waleta fujo wachache hadi kusababisha
kutolipa pela kwa kuwa wanadhani kuwa Tanga Cement ni dhaifu”.
Endapo jambo hili litafanikiwa, naamini faida zitakuwa nyingi kuliko hasara tofauti na
wengine ambao sio wahusika wanavyodhania wafanyakazi wa Tanga Cement wana shauku
kubwa ya mabadiliko haya.
Kuna mabadiliko ya hali yaliyopelekea Scancem International Da kuwasilisha ombi lingine la
ununuzi baada ya yale maamuzi yaliyofanywa mwaka 2022. Ninaunga mkono kwa dhati
mamlaka yaliyoruhusu mnunuzi huyu kuwasilisha upya ombi lake kutokana na mabadiliko
yanayoonekana yalitokea katika ya kipindi cha awali na hiki cha sasa ambacho ni kipya.
Baada ya uwasilishaji wa ombi jipya 2023, FCC ilitoa idhini ya uuzwaji kutokana na sababu
mpya zilizowasilishwa.
Scancem International Da, itaendelea kuonesha nia yake ya ununuzi wa Tanga Cement
lengo likuwa ni kuchangia ukuaji wa sekta ya simenti na uchumi kiujumla.
Uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 150 ndani ya Tanga Cement uko mbioni kufanyika huu ni
uthibitisho kwamba kiwanda kitaendelea na uzalishaji pamoja na kupanua uendeshaji wake.
Wafanyakazi hawatapunguzwa kazi na watapata uhakika zaidi wa kazi zao kuliko sasa.
Tangu kutangazwa kwa ombi la kwanza, bei za hisa ziliongezeka maradufu na pia
inatarajiwa kuongezeka zaidi ya hapo awali pale mpango huu utakapokamilika.
Ni dhahiri kwamba Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Tanga Cement wanfanyakazi
kubwa katika kufanikisha mpango huu na itakumbukwa kuwa ni moja ya miamala mikubwa
ya DSE kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu alisema.