Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Maabara ya TEHAMA na Vifaa vya TEHAMA kwa walimu 20 waliopata mafunzo ya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Kimbiji Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
………………………………………….
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 20/4/2023 imekabidhi vifaa vya kielektroniki kutoka nchini Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) pamoja na uzinduzi wa maabara ya TEHAMA kwa shule ya Sekondari ya Kimbiji mkoani Dar es salaam.
KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa walimu 20 wa shule ya Sekondari Kimbiji.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET , Dkt. Aneth Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini ambapo ameeleza kuwa walimu katika shule hiyo wataweza kutekeleza kwa urahisi kazi ya ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya kieletroniki.
Dkt. Komba amewataka walimu hao kuhakikisha wanaleta matokeo chanya ambayo yatasaidia katika uboreshaji wa elimu na ufaulu wa wanafunzi Kwa pamoja
“Mkayatumie mafunzo vizuri na vifaa hivyo mlivyokabidhiwa kwa kuleta matokeo chanya na tuone ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa Sekondari ya Kimbiji ,Amesema Dkt.Komba
Tukio hilo liliambatana na kukabidhi vishikwambi 20 kwa walimu walioshiriki programu ya mafunzo hayo.
Kwa upande wake , Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kimbiji Kigambomi Bi.Joyce Ndoane ameshukuru kutolewa kwa mafunzo hayo pamoja na vifaa vilivyotolewa ambapo amesema ana imani yataleta tija katika shule yake.
Vifaa vilivyokabihiwa ni TET ni vifaa vya TEHAMA kama Ups 26, Kompyuta (System Unit) 25, Computer Monitor 25, Projector 1, Scanner 1, Printer 1, Wireless Keyboard 35, Wireless Mouse 35, Hadphone 25, Electric Board (Projector Screen) 1, Web Camera 26, Digital Podium 1, Wired Keyboard 25, Wired Mouse 25, Desktop Speaker 26, Adapter 49 na Usb Flash 64-Gb 50.
Kwa niaba ya Serikali na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mkurugenzi Mkuu wa TET , Dkt. Aneth Komba ameishukuru nchi ya Korea Kusini kupitia Gwangju Metropolitan of Education (GMOE) kutoa mafunzo na vifaa vya TEHAMA nchini Tanzania. Jukumu letu kama jumuia ya Shule ya Sekondari Kimbiji ni kuvitunza vizuri vifaa vilivyokabidhiwa na hatimaye kufikia lengo lililokusudiwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akikabidhi cheti na vifaa vya TEHAMA kwa mwalimu Agnes Lazaro Kalondo wa shule ya Sekondari Kimbiji mara baada ya kumaliza mafunzo ya TEHAMA yaliyotolewa kwa walimu 20 wa sekondari hiyo na Taasisi ya Elimu Tanania TET na Mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) kutoka nchini Korea Kusini katikati ni Dkt. Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala TET na kushoto Joyce Ndaona Mkuu wa shule ya Sekodari Kimbiji.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akikabidhi cheti na vifaa vya TEHAMA kwa mwalimu Amina Halifa Mleli wa shule ya Sekondari Kimbiji mara baada ya kumaliza mafunzo ya TEHAMA yaliyotolewa kwa walimu 20 wa sekondari hiyo na Taasisi ya Elimu Tanania TET na Mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) kutoka nchini Korea Kusini katikati ni Dkt. Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala TET.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akikabidhi cheti na vifaa vya TEHAMA kwa mwalimu Amina Hassan Lubuva wa shule ya Sekondari Kimbiji mara baada ya kumaliza mafunzo ya TEHAMA yaliyotolewa kwa walimu 20 wa sekondari hiyo na Taasisi ya Elimu Tanania TET na Mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) kutoka nchini Korea Kusini katikati ni Dkt. Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala TET.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akikabidhi cheti na vifaa vya TEHAMA kwa mwalimu Hamida Hemedi wa shule ya Sekondari Kimbiji mara baada ya kumaliza mafunzo ya TEHAMA yaliyotolewa kwa walimu 20 wa sekondari hiyo na Taasisi ya Elimu Tanania TET na Mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) kutoka nchini Korea Kusini katikati ni Dkt. Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala TET.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akikabidhi cheti na vifaa vya TEHAMA kwa mwalimu Joyce Ndaona ambaye ni Mkuu wa shule ya Sekondari Kimbiji mara baada ya kumalia mafunzo ya TEHAMA yaliyotolewa kwa walimu 20 wa sekondari hiyo na Taasisi ya Elimu Tanania TET na Mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) kutoka nchini Korea Kusini katikati ni Dkt. Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala TET.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akikabidhi cheti na vifaa vya TEHAMA kwa mwalimu Mkolo Dockson Mlongwa ambaye ni Mkuu wa shule ya Sekondari Kimbiji mara baada ya kumalia mafunzo ya TEHAMA yaliyotolewa kwa walimu 20 wa sekondari hiyo na Taasisi ya Elimu Tanania TET na Mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) kutoka nchini Korea Kusini katikati ni Dkt. Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala TET.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET , Dkt. Aneth Komba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maabara ya TEHAMA katika shule ya Sekondari Kimbiji iliyotolewa kwa shule hiyo na Taasisi ya Elimu Tanania TET kwa kushirikiana na Mradi wa KLIC 2022 (Korean E-learning Improvement Cooperation 2022) kutoka nchini Korea Kusini katikati ni Dkt. Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala TET.
Muonekano wandai wamaabara hiyo ya TEHAMA.
Picha ya pamoja.